ZIFAHAMU SHERIA 7 ZA KIMATAIFA ZINAZOONGOZA VITA DUNIANI

Kumekuwa na matendo yaliyozoeleka kufanywa kwenye vipindi vya vita toka enzi za kale lakini ni kwa miaka takriban 150 iliyopita ndipo mataifa mbalimbali yalikubali kuweka Sheria za Kimataifa za Kudhibiti Athari za Vita na Migogoro ya Silaha kwa sababu za kibinadamu. Mkataba wa Geneva Mkataba wa The Hague ni mifano katika hili. Mara nyingi inajulikana kama “Sheria ya Kimataifa ya Kibinadamu (IHL),” lakini hujulikana pia kama “Sheria ya Vita” au “Sheria ya Mgogoro wa Silaha.”
Sheria ya Kimataifa ya Kibinadamu ni miongoni mwa sehemu ya sheria za kimataifa zinazohusika na kusimamia uhusiano kati ya nchi na nchi. IHL inalenga kudhibiti athari zinazoletwa na mapambano ya silaha kwa sababu za kibinadamu. Inalenga kulinda haki za watu ambao hawajawahi kuhusika au waliocha kuhusika na mgogoro huo, wagonjwa na majeruhi, wafungwa pamoja na wananchi, na kuelezea haki na wajibu wa kila upande unaohusika kwenye mgogoro huo juu ya watu wengine wasio vitani.
Kwakuwa ni Sheria, IHL imeweka utaratibu kwa pande mbili zilizo kwenye mgogoro wa kivita sio tu kwamba wanatakiwa kuhakikisha waniheshimu Sheria hiyo, bali pia wanawajibika kuheshimiana. Kwa mujibu wa Sheria hii, nchi hairuhusiwi kufumbia macho uhalifu wa kivita unaofanywa na jeshi lake au la mahasimu wake.
Mkataba wa Geneva na makubaliano mengine yaliyoongezwa umeweka masharti yafuatayo kwenye vita:
  1. Wanajeshi wanaojisalimisha kwa jeshi la upinzani au ambao wameshindwa kuendelea na mapambano kutokana na majeraha wanastahili kuheshimiwa uhai wao na kuhakikisha wanakuwa kwenye afya nzuri. Ni kosa kubwa sana kuwaua au kuwajeruhi mateka wa aina hii.
  2. Wagonjwa na majeruhi waliokamatwa na jeshi la upinzani wanatakiwa kukusanywa na kuhudumiwa. Ulinzi unatakiwa uwekwe kwa madaktari, nyumba zao, usafiri wao pamoja na vifaa vyao. Nembo ya Msalaba Mwekundu ni ishara ya ulinzi wao na ni lazima iheshimiwe na pande zinazopingana.
  3. Uhai na haki za msingi wa wanajeshi waliokamatwa (mateka) unatakiwa uheshimiwe. Ni lazima walindwe dhidi ya matendo yote ya kikatili na unyanyasaji. Wana haki ya kuwasiliana na familia zao na kupewa unafuu wa maisha wawapo matekani.
  4. Wananchi walio chini ya mamlaka ya jeshi la upinzani au chini ya jeshi la nchi nyingine wanastahili kuheshimiwa uhai wao pamoja na haki zao za kibinadamu.
  5. Kila mmoja ana haki ya kupata msaada wa kisheria. Hakuna mtu anayetakiwa kufungwa bila kesi yake kusikilizwa kwenye mfumo rasmi wa Mahakama. Hakuna anayetakiwa kuwa hatiani kwa kosa ambalo hakulifanya. Hakuna anayetakiwa kuadhibiwa kimwili au kiakili, adhabu ya kifungo, za mwili au adhabu yoyote ya kikatili.
  6. Pande zinazohusika kwenye mgogoro pamoja na wanajeshi wao hawana uhuru usio na mipaka juu ya mbinu au matendo yao wawapo vitani. Ni marufuku kutumia silaha au mbinu za kivita kusababisha hasara au mateso yasiyo na ulazima.
  7. Pande zinazohusika kwenye mgogoro huo lazima wakati wote waweze kutofautisha kati ya wananchi wa kawaida na wanajeshi ili kuwaacha raia pamoja na mali zao wakiwa salama. Tahadhari ya hali ya juu inatakiwa ichukuliwe kabla ya kufanya au kuruhusu mashambulizi yoyote ya kivita.
Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu inahesabika kama “rafiki” wa mkataba wa Geneva pamoja na mikataba mingine inayolinda sheria za kimataifa za kibinadamu. Hata hivyo, haiwezi kufanya kazi kama polisi au Hakimu kwa upande wowote unaohusika kwenye mgogoro. Kazi hii ni ya Serikali husika ambazo pia ni wanachama wa mikataba hii. Serikali hizi pia ndio zinazohusika na kuwaadhibu wahusika wa uhalifu wa kivita uliofanywa kwenye mgogoro husika.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post