Askofu Niwemugizi aacha gumzo la Katiba mpya

SHARE:

Dar es Salaam. Hoja ya Askofu Severin Niwemugizi kuwa yuko tayari kuitwa mchochezi kutokana na msimamo wake wa kutaka Katiba Mpya, imeach...Dar es Salaam. Hoja ya Askofu Severin Niwemugizi kuwa yuko tayari kuitwa mchochezi kutokana na msimamo wake wa kutaka Katiba Mpya, imeacha mjadala kwa wachambuzi wa masuala ya kisiasa.
Wapo wanaoona kuwa suala la kuandika Katiba Mpya liachwe kwa Serikali na wengine wanamuunga mkono rais huyo wa zamani wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC).
Baadhi ya wanaotofautiana naye wanasema hoja yake inaonekana kuwa ya uanaharakati zaidi, lakini wanaomuunga mkono wanasema ana uhuru na haki kwa asilimia 100 kuongeza uzito wa kushawishi kufufuliwa kwa mchakato wa kuandika Katiba Mpya.
Hata hivyo, Rais Magufuli ameshasema kuwa Katiba Mpya si kipaumbele chake na wala hakuwahi kutaja suala hilo wakati wa kampeni zake.
Miongoni mwa wachambuzi waliopinga hiyo ni Profesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Benson Bana.
“Baba Askofu yupo sahihi ila ajue Katiba si mwarobaini wa changamoto za kijamii kama haitasimamiwa ipasavyo,” alisema Profesa Bana alipohojiwa kuhusu hoja hiyo.
“Inaweza (Katiba) ikawepo na watawala wakaikiuka vilevile. Tunachotaka ni umakini na nia njema katika kuisimamia.”
Alisema mambo mengi ya kiutendaji anayoyafanya Rais Magufuli yapo kwenye Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyopongozwa na Jaji Joseph Warioba .
“Mimi mwenyewe ni muumini wa rasimu ya Jaji Warioba. Sasa kinachotakiwa kufanyika ni kuendelea na mchakato wa kuipigia kura au kuileta ile ya Jaji Warioba ambayo maoni yake mengi yalibadilishwa,” alisisitiza.
Hata hivyo, alisema alimuelewa Rais Magufuli aliposema mchakati huo si kipaumbele chake kwa sasa.
“Kuchagiza ni jukumu letu wote, lakini tusipelekwe. Namuelewa Rais Magufuli.”
Lakini mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Iringa (UoI), Dk Jimson Sanga alisema kama kiongozi wa dini, Askofu Niwemugizi ametumia haki yake msingi kikatiba kukumbushia mchakato huo aliouita muhimu.
“Ana haki ya kutoa maoni yake kama Mtanzania wa kawaida, anaweza hata kuomba kukutana na Rais ili akazungumze naye kuhusu hilo,” alisema Dk Sanga.
“Ni kiongozi mwenye dhamana ya kulinda amani kwa misingi ya maombi.”
Alisema kuna umuhimu mkubwa wa kuendelea kushawishi mchakato huo kwa sababu itasaidia kuongoza nchi kulingana na wakati uliopo.
“Ni lazima makundi mbalimbali tukiwamo wanazuoni tushawishi suala hili,” alisema Dk Sanga.
Juhudi za mwandishi wetu kupata maoni ya vyama vya siasa kuhusu suala hilo, ziliishia upande mmoja kwani katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, Humphrey Polepole alisema hawezi kulizungumzia kwa sasa kwa kuwa chama hicho kinaendelea na vikao vya juu.
Lakini mkurugenzi wa itikadi na mambo ya nje wa Chadema, John Mrema alisema hofu ya Askofu Niwemugizi ya kutoa maoni hasa yanayoilenga Serikali moja kwa moja ni ya wengi.
Mrema alisema kauli ya askofu huyo imekuja wakati muafaka kwa sababu msimamo wa chama hicho ni kufufuliwa kwa mchakato huo ili kupatikana kwa Katiba itakayotibu matatizo mengi yaliyopo.
“Sisi tunataka rasimu ya Jaji Warioba kwa sababu hiyo ndiyo itakayotibu matatizo mengi,” alisisitiza.
Alimtaka Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi kufufua mchakato huo kwa sababu alishiriki na alikuwa miongoni mwa wajumbe waliotengeneza Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Tume ya Jaji Warioba.
“Tunamtaka Profesa Kabudi arejeshe mchakato kwa sababu yeye alikuwepo,” alisema.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: Askofu Niwemugizi aacha gumzo la Katiba mpya
Askofu Niwemugizi aacha gumzo la Katiba mpya
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/09/askofu-niwemugizi-aacha-gumzo-la-katiba.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/09/askofu-niwemugizi-aacha-gumzo-la-katiba.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy