BAADA YA MAKINIKIA KUZUIWA, ACACIA YATANGAZA PIGO JINGINE KWA WATANZANIA

Kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia imetangaza azma ya kupunguza utendaji kazi wake katika mgodi wa Bulyanhulu ambao ni mmoja wa migodi inayomiliki kutokana na kuongezeka kwa gharama za uendeshaji wa mgodi huo.
Kampuni hiyo imeeleza kwamba, tangu kuzuiwa kwa usafirishaji wa mchanga wa madini (makinikia) nje ya nchi mwezi Machi mwaka huu, imekumbwa na hasara kubwa iliyopelekea kushuka kwa uzalishaji na hivyo kusudio lao la kupunguza utendaji kazi ni ili kuweza kukabiliana na mazingira ya sasa.
Katika taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya kampuni hiyo, Acacia imesema kuzuiwa kwa makinikia tangu Machi hadi leo kumesababusha hasara ya 35% ya uzalishaji wao wa mwaka.
Aidha, wameeleza kwamba, changamoto mbalimbali za kiutendaji walizokumbana nazo zimeisababishia kampuni hiyo hasara ya dola za kimarekani 210 milioni sawa na Tsh 470.8 bilioni.
Acacia wamesema watapunguza utendaji kazi pamoja na matumizi katika mgodi huo endapo zuio la kusafirisha makinikia nje ya nchi halitaondolewa kuelekea miwsho robo ya tatu ya mwaka 2017.
Wameeleza lengo la kufanya hivyo ni kuweza kukabiliana na mazingira ya sasa ili waweze kuendelea na uzalishaji katika kipindi kirefu.
Kuhusu mazungumzo yanayoendelea sasa kati ya Barrick Gold na Serikali, Acacia wamesema kwamba wanayaunga mkono na kwamba wanaamini uamuzi utakaofikiwa utakuwa ni wa manufaa kwa pande zote.
Hapa chini ni taarifa rasmi iliyotolewa na kampuni hiyo;
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post