BI MWENDA KUZIKWA KESHO


Naibu Katibu Mkuu wa CUF, upande wa Profesa Ibrahim Lipumba, Magdalena Sakaya amesema chama hicho kimepokea kwa masikitiko kifo cha Mbunge mteule wa Viti Maalum Hindu Mwenda
Hindu alifariki dunia ghafla jana nyumbani kwake Kibada Kigamboni na anatarajiwa kuzikwa kesho saa 7 mchana katika makaburi ya Kisutu wilayani Ilala,  Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza, leo Jumamosi Septemba 2 Sakaya amesema  Hindu alikuwa ni mpambanaji  na mtu mwenye kukijenga chama hicho  kuanzia miaka ya 90  hivyo ni pigo kubwa kuondoka kwake.
‘’Hata ukifika  Tabora leo hii hakuna mwanachama wa CUF asiyemjua Hindu’ ’amesema Sakaya.
“Sijui niseme nini maana zilikuwa zimebaki siku chache tu aende Dodoma kuapishwa baada ya kuteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) mwezi uliopita,” amesema Sakaya ambaye pia ni Mbunge wa Kaliua Tabora.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post