BREAKING: TUNDU LISSU APIGWA RISASI AKIWA DODOMA

Habari za kusikitisha zilizotufikia muda huu zinaeleza kuwa Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu amepigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa mkoani Dodoma.
Taarifa iliyochapishwa katika ukurasa wa Facebook na wa Twitter wa Mbunge mwenzake, Zitto Kabwe zinaeleza kuwa amepigwa risasi nyingi.
“Mbunge mwenzetu wa Singida Mashariki amepigwa risasi nyingi na watu wasiojulikana. Kakimbizwa hospitali Dodoma,”- ameandika Zitto.
Taarifa za awali zinadai kuwa, Tundu Lissu ambaye ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA amepigwa risasi takribani tatu akiwa nyumbani kwake eneo la Area D, Dodoma.
Viongozi mbalimbali wa vyama vya serikali wamefika hospitali baada ya kupata taarifa za Lissu kupigwa risasi.
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka hospitalini Dodoma, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema kwamba Tundu Lissu alipigwa risasi kutoka kwenye gari lililokuwa likimfuata kwa nyuma.
Mbowe ameeleza kwamba risasi hizo zilitoka katika bunduki aina ya Sub-Machine Gun (SMG).
Taarifa kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma na Daktari zimeeleza kuwa Tundu Lissu ameshambuliwa maeneo ya tumboni na mguuni na kwamba bado yupo hai.
Picha za gari aliyokuwa akilitumia Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu likionyesha maeneo yaliyopigwa risasi.Mwenyekiti wa CHADEMA akiwa na mtu mmoja aliyeshika nguo zinazoaminika kuwa Tundu Lissu alikuwa amezivaa kabla ya kushambuliwa kwa risasi.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post