BUNGE LAPITISHA MUSWADA WA KUANZISHA SHIRIKA JIPYA LA RELI (TRC)

SHARE:

Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha muswada wa sheria ya reli ya mwaka 2017 (The R...

Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha muswada wa sheria ya reli ya mwaka 2017 (The Railways Act, 2017) ambao unapendekeza kuanzisha Shirika la Reli Tanzania (TRC) litakalokuwa na jukumu la kusimamia, kuendeleza miundombinu ya reli na kutoa huduma ya usafiri wa reli.
Akiwasilisha muswada huo leo Bungeni, Mjini Dodoma Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema kuwa dhumuni ya muswada huo ni kuweka mfumo madhubuti wa utoaji huduma ya usafiri wa reli, usimamizi na uendelezaji wa miundombinu ya reli.
“Muswada huu unaainisha utaratibu wa kuhamisha watumishi kutoka Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) na Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli Nchini (RAHCO) kwenda katika Shirika jipya,” alisema Prof. Mbarawa.
Vile vile amesema kuwa muswada huo pia unaainisha vyanzo vya mapato ambavyo ni pamoja na mfuko wa reli, ruzuku toka Serikalini, nauli za abiria pamoja na uhifadhi wa eneo la reli.
Prof. Mbarawa amesema kuwa TRL ilikuwa ikisimamia masuala ya usafiri wa gari moshi (treni) na RAHCO ilikuwa ikisimamia miundombinu. Aidha amesema kipindi chote ambacho taasisi hizo zimetenganishwa katika utendaji kazi kumesababisha kushuka kwa mapato na utendaji wa TRL.
Kushuka kwa mapato kumetokana na RAHCO kutokuwa tayari au kuchelewa kurekebisha miundombinu hivyo kusababisha kukwama kwa safari mara kwa mara.
Aidha amesema kuwa, Serikali imechagua Shirika kuitwa TRC kutokana na namna ambavyo Watanzania waliliamini shirika hilo kabla ya kubadilishwa jina kwenda TRL ambapo kumekuwa na changamaoto nyingi  ikilinganishwa na hapo awali.
“Shirika jipya la TRC litakuwa na ubora zaidi ukilinganisha na ilivyokuwa TRL na TRC ya zamani,” alifafanua Prof. Mbarawa.
Vile vile amesema kuwa wafanyakazi watakao hamishwa kwenda shirika jipya watalipwa stahili zao na hata wale watakaohamishwa kwenda katika taasisi, serikali au kuachishwa kazi pia haki zao zitaangaliwa.
Naye, Mbunge wa Kaliuwa kwa tiketi ya CUF Magdalena Sakaya ameishauri Serikali kuongeza mabehewa kutokana na wananchi wengi kushindwa kutumia usafiri huo kwa sababu ya uchache wa mabehewa.
Hata hivyo amesema kuwa reli ndio usafiri pekee ambao ni wa uhakika kwa wananchi wenye hali ya chini pamoja na mizigo.
Serikali iliingia mkataba na Rites mwaka 2006 ambao ulisababisha kuvunjwa kwa TRC na kuunda TRL ambapo Serikali ilikuwa na uwekezaji wa asilimia 49.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,73,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,273,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,13,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,567,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3301,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,333,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,386,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,68,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1379,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1286,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: BUNGE LAPITISHA MUSWADA WA KUANZISHA SHIRIKA JIPYA LA RELI (TRC)
BUNGE LAPITISHA MUSWADA WA KUANZISHA SHIRIKA JIPYA LA RELI (TRC)
https://4.bp.blogspot.com/-xZxVlA_yc9U/WblvUOdvbtI/AAAAAAAAeq0/1fwWZzw-SoMC3QHPsDnOsLHlHCW8i6BsACLcBGAs/s1600/xkati-750x375.jpg.pagespeed.ic.OCScE_B1iZ.webp
https://4.bp.blogspot.com/-xZxVlA_yc9U/WblvUOdvbtI/AAAAAAAAeq0/1fwWZzw-SoMC3QHPsDnOsLHlHCW8i6BsACLcBGAs/s72-c/xkati-750x375.jpg.pagespeed.ic.OCScE_B1iZ.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/09/bunge-lapitisha-muswada-wa-kuanzisha.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/09/bunge-lapitisha-muswada-wa-kuanzisha.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy