Canada, Unicef, Tigo wawezesha kasi uandikishaji vyeti vya watoto

SHARE:

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara kutumia fursa waliyoipa...

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara kutumia fursa waliyoipata ya usajili na utoaji vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wa umri chini ya miaka mitano kufanya hivyo kwa maslahi ya watoto na taifa.

Dkt. Mwakyembe alisema hayo wakati akizundua mpango huo wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara.

Alisema uandikishaji wa watoto utasaidia kuwa na rekodi sahihi ya idadi ya vizazi na vifo ambapo inasaidia serikali katika kuangalia mipango yake na mahitaji ya wananchi katika masuala ya afya, jamii na uchumi.

Aidha vyeti vinavyopatikana pamoja na kuonesha utambuzi wa mtoto, pia vinamsaidia kumpatia haki zake nyingine kwa mujibu wa sheria.Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (mwenye kofia ya pama) akiwasili na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi wakati wa uzinduzi wa mpango wa usajili na utoaji vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wa umri chini ya miaka mitano uliofanyika wilayani Tandahimba mkoani Mtwara.Akihutubia katika uzinduzi wa kampeni hiyo ambayo kauli mbiu yake ni Mtoto anastahili cheti za kuzaliwa, mpe haki yake ya kuzaliwa, Waziri Mwakyembe alisema kwamba kampeni hiyo kwa mikoa ya Mtwara na Lindi inatarajia kuwanufaisha watoto zaidi ya 290,000 wenye umri chini ya miaka mitano.

Akihutubia kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi ambaye shughuli hiyo iko katika mkono ya ofisi yake alisema kwamba wananchi wa Lindi na Mtwara walikuwa nyuma katika usajili kama walivyokuwa watu wa Njombe na kutumaini watafanya vyema kama wananchi wenzao walivyofanya.

Wananchi wa Njombe kabla ya kampeni walikuwa wameandikisha kwa asilimia 8.9 toka Uhuru upatikane lakini baada ya kuanza kwa kampeni katika kipindi cha miezi mitatu wamefikia asilimia 99.Mwakilishi wa UNICEF nchini, Maniza Zaman akisalimia wakazi wa wilaya ya Tandahimba (hawapo pichani) wakati wa zoezi la utambulisho kwenye hafla ya uzinduzi wa mpango wa usajili na utoaji vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wa umri chini ya miaka mitano uliofanyika wilayani Tandahimba mkoani Mtwara.Kampeni ya kuandikisha vyeti watoto chini ya miaka mitano imelenga kuondoa kero za uandikishaji na kuweka sawa mfumo wa uandikishaji wa vizazi na vifo hivyo kusaidia mipango ya serikali kwa kuwa na takwimu halisi na hivyo kupanga maendeleo halisi.

Mpango huo uliozinduliwa jana unafikisha huduma ya usajili karibu na wananchi kwa kuanzisha vituo vya usajili katika vituo vya afya ambavyo pia ndio vinavyosaidia elimu ya afya ya uzazi, kiliniki na uzazi.

Pia vituo hivyo vya usajili vitakuwepo katika ofisi za kata, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya taifa ya ugatuaji madaraka.Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea na Wakazi wa Wilaya ya Tandahimba Mkoani Mtwara (hawapo pichani) wakati wa Uzinduzi wa mpango wa usajili na utoaji vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya umri miaka mitano kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara.Kueplekewa kwa vituo hivyo katika mtindo huo kutawafanya wazazi kuwa na vituo 7809 vya kuandikisha watoto ukilinganisha na vituo kumi vilivyokuwepo awali.

Pia imeelezwa kuwa kutakuwa na watendaji 1,500 waliofunzwa namna ya kuandikisha vyeti.

Pia ili kufanikisha zoezi hilo serikali imeondoa ada ya usajili kwa watoto wa miaka chini ya mitano.

Uandikishaji huo utatumia teknolojia ya simu na hivyo kuwa rafiki zake katika ukusanyaji wa takwimu.Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Bibi Emmy Hudson akitoa maelezo mafupi kuhusu hafla ya uzinduzi wa mpango wa usajili na utoaji vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya umri miaka mitano kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara uliofanyika wilayani Tandahimba.Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Bibi Emmy Hudson amesema kwamba mfumo unaotumika sasa utachagiza uandikishaji wa watoto na kuwapatia vyeti vyao vya kuzaliwa baada ya shughuli hiyo kusuasua kwa muda mrefu.

“Tunafanya mabadiliko makubwa katika mfumo ili iwe rahisi kwa watoto na familia zao kupata vyeti vya kuzaliwa,” anasema Hudson.

Aidha alisema kwamba mfumo huo mpya wa uandikishaji umesaidia maelfu ya wazazi kuwapatia vyeti vya kuzaliwa watoto wao katika maeneo ambayo tayari unafanyakazi.Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri RITA, Prof Hamisi Dihenga akitoa maelezo kuhusu hali ya usajili na mpango wa usajili wa watoto walio na umri chini ya miaka mitano wakati wa hafla ya uzinduzi wa mpango huo iliyofanyika wilayani Tandahimba mkoani Mtwara.Pia alishukuru Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto la UNICEF, Kampuni ya simu ya mkononi ya Tigo na Serikali ya Canada kwa kutoa mchango mkubwa katika kufanikisha mfumo huo mpya wa uandikishaji.

Mwakilishi wa UNICEF nchini Tanzania Bi Maniza Zaman alisema kwamba kila mtoto ana haki ya kuandikishwa na kupewa cheti chake cha kuzaliwa. Alisisitiza kwamba cheti za kuzaliwa ni rekodi sahihi ambayo mtoto anahitaji wakati akizaliwa.

Alisema kampeni ya sasa itawaingiza katika rekodi mamilioni ya watoto ambao hawaonekani na hivyo kusaidia watoto kupata haki zao.Mwakilishi wa UNICEF nchini, Maniza Zaman akitoa salamu za shirika lake kwa wakazi wa wilaya ya Tandahimba wakati wa uzinduzi wa mpango huo katika mikoa ya Mtwara na Lindi.Pamoja na watoto kupata haki zao, serikali pia inakuwa na uwezo wa kutambua idadi ya watoto na kuweka mipango madhubuti ya kuwainua.

Uzinduzi wa mpango huo kwa mikoa ya Mtwara na Lindi unaongeza zaidi idadi ya mikoa ambayo imefikiwa.

Mikoa ya Lindi na Mtwara inaingia katika mikoa 7 ambayo tayari imefikiwa tangu mpango huo uanze mwaka 2012 kwa msaada wa fedha za serikali ya Canada. Mikoa hiyo ni Geita, Shinyanga, Mbeya, Songwe, Mwanza, Iringa na Njombe.Unadikishaji watoto katika mikoa hiyo tayari umefikia milioni 1.64 walio chini ya miaka mitano.Mwakilishi wa Ubalozi wa Canada, Dr. Madani Thiam akizungumza kwa niaba ya Balozi wa Canada nchini Ian Myles wakati wa uzinduzi wa mpango huo uliofanyika wilayani Tandahimba mkoani Arusha.Balozi wa Canada nchini Ian Myles akizungumza kwa niaba ya serikali ya nchi yake amesema kwamba itaendelea kufadhili mpango huo kutokana na wao kuamini katika haki za mtoto ikiwamo upatikanaji wa cheti chake cha kuzaliwa na takwimu kusaidia serikali kutekeleza wajibu wake kwa watoto ikiwamo masuala ya afya na elimu.

Fedha zilizotolewa zimelenga kusaidia kuandikisha watoto milioni 3.5 chini ya umri wa miaka mitano.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari alisema kampuni yake imeunga mkono shughuli hiyo kwa kutambua umuhimu wake na pia katika matumizi ya teknolojia kurahisisha maisha ya wananchi.Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mpango wa usajili na utoaji vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya umri miaka mitano kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara.Alisema Tigo inatoa mchango wake kwa kuweka aplikesheni inayotakiwa ambayo inatendakazi kwa haraka na ukamilifu.

Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 inaonesha kwamba ni asilimia 13 tu ya watoto chini ya miaka mine wana vyeti vya kuzaliwa huku Tanzania Bara ikiwa chini ya asilimia 12.

Wakizungumza katika uzinduzi huo wananchi wameelezea kufurahishwa kwao kwa kusogezewa huduma karibu ili waweze kuitumia.

Zuwena Abdallah Mawazo ambaye alifika na mtoto wake alisema amefurahishwa sana na serikali kuleta huduma hiyo ambayo amesema imeondolewa usumbufu wa njoo leo nenda kesho.Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Prof. Sifuni Mchome akizungumza kwenye uzinduzi wa mpango huo ambapo amesema kwamba kama Wizara wana wajibu wa kufikisha huduma hiyo kwa wananchi hususani kwa wananchi ambao wako maeneo ya mbali bila kujali hali yao ya kimaisha huku akisisitiza kwamba kila mtoto atapatiwa haki hiyo ya kuandikishwa na kupewa cheti.Alisema kwamba hatua walioifanya serikali ni ya muhimu kwani hataki mtoto wake kuja kusumbuka baadae kutafuta huduma mbalimbali kwa kutokuwa na cheti cha kuzaliwa.

Aidha alisema kwamba amefurahishwa na kuondolewa kwa tozo na kutaka wazazi wenzake kuwafikisha watoto ili wapatiwe vyeti vya kuzaliwa.

Mkazi mwingine wa Tandahimba ambaye alijitambulisha kwa jina la maarufu Fumao Kavahana alisema kwamba amefika kumwandikisha mtoto wake wa miaka miwili ili kuondokana na usumbufu wa baadae.Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiwatambulisha wadau wa maendeleo waliowezesha mpango huo ambao ni Canada, Unicef na Tigo kwa wakazi wa wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara.Aidha alisema kwamba amefika pale na mtoto wake huyo kwa kuwa yeye na mzazi mwenzake wametengana lakini alimfikishia mtoto ili ampeleke kuandikishwa wakati yeye akienda kumsaidia baba yake kulima Korosho Manyanga.

Fumao mwenye umri wa miaka 36 alisema kwamba alikuwa na mtoto mwingine wa miaka 11 ambaye hajamwandikisha na kwamba anatarajia kuchukua hatua hapo baadae za kumwandikisha.

Aidha alitoa wito kwa wanaume wenzake kuhimiza watoto waandikishwe na kuwasaidia wanawake kazi hiyo kwa kuwa watoto ni wawote.Wadau wa maendeleo Canada, Tigo pamoja na Unicef katika hafla ya uzinduzi wa mpango wa usajili na utoaji vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya umri miaka mitano kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akikata utepe katika kitabu cha usajili pamoja na simu kuashiria uzinduzi wa mpango wa usajili na utoaji vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya umri miaka mitano kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri RITA, Prof Hamisi Dihenga.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akionyesha Kitabu cha Usajili pamoja na Simu kuashiria uzinduzi wa mpango wa usajili na utoaji vyeti vya kuzaliwa kwa watoto waliochini ya umri miaka mitano kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri RITA, Prof Hamisi Dihenga.Mwakilishi wa UNICEF nchini, Maniza Zaman (katikati) akipongezwa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi (kulia) huku mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (mwenye kofia ya pama) akishuhudia tukio hilo.


Kaimu Mkurugenzi wa Sheria Rita, Lina Msanga akitoa maelezo kwa mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe wakati wa zoezi la usajili kwa vitendo kwenye uzinduzi wa mpango wa usajili na utoaji vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya umri miaka mitano kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara.Mkazi wa Tandahimba ambaye alijitambulisha kwa jina la maarufu Fumao Kavahana (36) alipowasili na mtoto wake wa miaka miwili kwenye zoezi hilo la bure la usajili na utoaji vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya umri miaka mitano kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara.


Mkazi wa wilaya ya Tandahimba Zuwena Abdallah Mawazo akiwa amejipumzisha na mtoto wake akisubiri usajili na utoaji vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya umri miaka mitano kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara.


Mfano wa cheti cha kuzaliwa kilichokamilika taarifa zote za muhimu za wazazi na mtoto.


Picha juu na chini ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (aliyevaa kofia ya pama) akiwakabidhi vyeti vya kuzaliwa wazazi kwa niaba ya watoto wao wenye umri chini ya miaka mitano wakati wa Uzinduzi wa Mpango wa Usajili na Utoaji Vyeti kwa Watoto waliochini ya Umri Miaka Mitano Wilayani Tandahimba, Mkoani Mtwara.

Zoezi la bure likiendelea la usajili na utoaji vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya umri miaka mitano kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara.


Kikundi cha ngoma ya Lipandula kikitoa burudani wakati wa uzinduzi wa mpango wa usajili na utoaji vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya umri miaka mitano kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara.


Watoto wa shule ya awali wilayani Tandahimba wakitoa burudani ya wimbo maalum wa kuhamasisha kauli mbiu ya “Mtoto anastahili cheti cha kuzaliwa mpe haki yake ya kuzaliwa” katika hafla ya uzinduzi wa mpango huo.


Baadhi ya waheshimiwa Wabunge wa mikoa ya Lindi na Mtwara na viongozi wengine wa mikoa hiyo walioshiriki uzinduzi wa mpango wa usajili na utoaji vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya umri miaka mitano kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara.


Sehemu ya wafanyakazi wa Unicef, Rita, Tigo na wageni waalikwa katika hafla ya uzinduzi wa mpango wa usajili na utoaji vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya umri miaka mitano kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara.


Baadhi ya wanafunzi wa shule za wilaya ya Tandahimba walioshiriki uzinduzi wa mpango wa usajili na utoaji vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya umri miaka mitano kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara.


Pichani juu na chini baadhi ya wazazi waliojitokeza na watoto wao katika hafla ya uzinduzi wa mpango wa usajili na utoaji vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya umri miaka mitano kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara.Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe katika picha ya pamoja na meza kuu.


Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe katika picha ya pamoja na waheshimiwa Wabunge wa mikoa ya Lindi na Mtwara.


Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe katika picha ya pamoja na viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama ya mikoa ya Lindi na Mtwara.


Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe katika picha ya pamoja na viongozi wa kata za wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara.


Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe na wafanyakazi wa Unicef na Tigo.


COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: Canada, Unicef, Tigo wawezesha kasi uandikishaji vyeti vya watoto
Canada, Unicef, Tigo wawezesha kasi uandikishaji vyeti vya watoto
http://www.thebeauty.co.tz/wp-content/uploads/2017/09/JA3A5101.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/09/canada-unicef-tigo-wawezesha-kasi.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/09/canada-unicef-tigo-wawezesha-kasi.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy