CCM YAMVUA UDIWANI YUSUF MANJI

Mfanyabiashara Yusuf Manji amepoteza sifa ya kuwa Diwani wa Kata ya Mbagala Kuu kutokana na kutohudhuria vikao zaidi ya sita na vikao vya kamati vya maendeleo ya halmashauri ya Temeke zaidi ya vitatu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Meya wa Manispaa ya Temeke, Abdallah Chaurembo amesema kutokana na sababu hizo, na kwa mujibu wa sheria, Manji amepoteza sifa ya kuendelea kuwa diwani.
Manji ameshindwa kuhudhuria vikao hivyo kutokana na kushikiliwa na Polisi katika kesi mbili zinazomkabili ambazo ni matumizi ya dawa za kuelvya pamoja na ile ya uhujumu uchumi.
Kuhusu kesi ya uhujumu uchumi, Manji pamoja na wenzake wanatuhumiwa kukutwa na vitambaa vinavyotumika kutengenezea sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) pamoja na mihuri ya jeshi hilo kinyume na sheria.
Kuhusu kesi ya dawa za kulevya, mshtakiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Februari 16, 2017 akidaiwa
kati ya Februari 6 na 9, 2017 katika eneo la Upanga Sea View wilayani Ilala alitumia dawa za kulevya aina ya heroin
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post