CHELSEA YAPAMBANA NA KUFANIKIWA KUIBUKA NA USHINDI DHIDI YA LEICESTER CITY

Chelsea imegangamala na kufanikiwa kuifunga Leicester City na kuwafanya mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu ya Uingereza kukwea nafasi ya tatu kwa ushindi wa tatu mfululizo.

Katika mchezo huo timu zote mbili zilihaha kutafuta goli na alikuwa Alvaro Morata aliyefunga goli la kwanza akinasa pasi ya Cesar Azpilicueta katika kipindi cha kwanza.

Wageni Chelsea waliongeza mashambulizi katika kipindi cha pili na alikuwa kiungo wa zamani wa Leicester N'Golo Kante, aliyefunga goli la pili.

Madhambi yaliyofanywa na Thibaut Courtois yaliisaidia Leicester kupatiwa penati ambayo ilipigwa na Jamie Vardy na kufunga goli pekee la Leicester.
Mchezaji mpya wa Chelsea Alvaro Morata akiruga juu kuupiga kichwa mpira uliozaa goli la kwanza
Kiungo N'Golo Kante akiachia shuti la umbali wa yadi 30 na kuifunga goli timu yake ya zamani
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post