DC MTATURU AWASIHI VIJANA KUDUMISHA NIDHAMU NA MSHIKAMANO

SHARE:

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya Siasa Wilaya akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu...

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne
Mtaturu ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya Siasa Wilaya akizungumza
na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya
ya Ikungi ulioketi kuchagua uongozi wapya watakaoiongoza jumuiya hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne
Mtaturu ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya Siasa Wilaya akizungumza
na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya
ya Ikungi ulioketi kuchagua uongozi wapya watakaoiongoza jumuiya hiyo.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya
ya Ikungi wakimsikiliza mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano huo 
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne
Mtaturu kabla ya 
kuchagua uongozi wapya kuongoza jumuiya hiyo ngazi ya Wilaya.
Mbunge wa Jimbo La Singida Magharibi Mhe Elibariki Kingu akizungumza
na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya
ya Ikungi ulioketi kuchagua uongozi wapya watakaoiongoza jumuiya hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne
Mtaturu (Mwenye shati la Njano) akifurahia jambo wakati wajumbe wa mkutano Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya hiyo wakiimba pamoja.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne
Mtaturu
 akisalimiana na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa
Vijana Wilaya ya Ikungi mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa mkutano.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne
Mtaturu
 akisalimiana na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa
Vijana Wilaya ya Ikungi mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa mkutano.
Mzee Jumanne Ally Ngaa akizungumza jambo wakati wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa
Vijana Wilaya ya Ikungi katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Ikungi.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne
Mtaturu
 (Mwenye shati la Njano), Mbunge wa Jimbo la Singida Mgharibi Mhe Elibariki Kingu (Wa Kwanza kushoto Pichani) na viongozi wengine wakifatilia Mkutano Mkuu wa Umoja wa
Vijana Wilaya ya Ikungi katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Ikungi.
Mbunge wa Jimbo La Singida Magharibi Mhe Elibariki Kingu akisalimiana na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Vijana Wilaya ya Ikungi mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa mkutano.
Mbunge wa Jimbo La Singida Magharibi Mhe
Elibariki Kingu akifurahia jambo wakati akisalimiana na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa
Vijana Wilaya ya Ikungi mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa mkutano.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya
ya Ikungi wakimlaki mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano huo 
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne
Mtaturu kabla ya 
kuchagua uongozi wapya kuongoza jumuiya hiyo ngazi ya Wilaya.
 

Na
Mathias Canal, Singida
 
Vijana wametakiwa
kusimamia misingi ya Nidhamu ndani na nje ya Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa
Chama Cha Mapinduzi kwa kuhuisha mshikamano ili kulinda misingi ya Utaifa na
uwajibikaji kwani wao ndio nguvukazi ya Taifa na ushindi wa Chama Cha Mapinduzi.
 
Kauli hiyo imetolewa na
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya siasa Wilaya wakati akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Ikungi kwenye mkutano
wa uchaguzi wa viongozi wa Jumuiya hiyo katika ukumbi wa shule ya Sekondari
Ikungi.
 
Mhe Mtaturu alisema kuwa Dhana ya
Demokrasia ni jambo muhimu linalohitaji kuheshimiwa na kuenziwa ndani ya Chama
na  Jumuiya zake hivyo kuimarisha nidhamu, mshikamano na upendo ndio
silaha pekee itakayoleta heshima ndani ya jumuiya ya vijana wa CCM ili iweze
kusonga mbele zaidi na kuwa na mafanikio makubwa katika kuimarisha kipato cha
vijana.
 
Alisema kuwa Nia ya UVCCM ni kujenga
na kudumisha haiba  njema ya kuendelea kuheshimu misingi ya demorasia ya
kweli, yenye kuchunga  adabu na kufuata nidhamu, miiko na maadili kwa kila
mwanachama anayetaka kutumia haki ya kuchagua au kuchaguliwa.
 
Alisema kuwa mkutano huo unapaswa
kuchagua viongozi waadilifu watakaohuisha misingi ya mshikamano na ujenzi wa
CCM Mpya ili kuondoa  malumbano yenye
kupandikiza chuki na kupalilia mifarakano isio na ulazima.
 
Alisema wapo baadhi ya vijana
wanatumia vibaya nafasi zao katika Jumuiya hiyo kwa kuwachafua wenzao kwenye
mitandao ya kijamii na wakati mwingine wapo wanaothubutu kuwatukana wenzao
matusi ya nguoni kinyume na ustaarabu, ubinadamu na misingi na Maadili ya Chama
Cha Mapinduzi.
 
Wapo baadhi yao hujivika kofia ya
Jumuiya wakitumia  njia hatari na batili, kwa kukebehi, kutuhumu wenzao
kinyume na utaratibu huku baadhi yao hata kufikia kutoa madai  yanayovuka
mipaka na  kubeba taswira ya  Jinai au  madai. 
 
“Ndugu zangu Kwa miaka yote
wanajumuiya na viongozi wote wa CCM wamekuwa wakiishi kwa kuzingatia misingi ya
Umoja, Upendo, mashauriano na kudumisha Maelewano hivyo nakushaurini nyote
kuvienzi ili kuwa na CCM Mpya itakayowaletea wananchi maendeleo na kuendelea kuongoza
dola” Alisema mHe Mtaturu
 
Mhe Mtaturu alisema Uchaguzi ni
kipimo cha kupevuka na kielelezo cha ukomavu wa demokrasia ya kweli bila
mizengwe au hila ndani ya chama na Jumuiya kwa lengo la kusimamia shabaha na
misingi sahihi itokanayo na miongozo, maelekezo na kuheshimu utaratibu
unaohimizwa na Chama Cha Mapinduzi .
 
Alisema Ili kuonyesha  kutii na
kufuata maelekezo yanayotolewa mara kwa mara na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Magufuli kila mwanachama
anapaswa kujitambua, kujiheshimu, kufuata misingi ya katiba na kuepukana na rushwa ili kulinda heshima ya Chama Cha Mapinduzi.
 
Mhe Mtaturu pia alizitaja fursa
zilizopo katika Wilaya ya Ikungi ambazo vijana wanaweza kuzitumia ili
kuimarisha kipato chao kuwa ni pamoja na Kilimo cha Korosho, Mpunga, Pamba na
Ufugaji wa kuku.
 
Pia aliwasihi vijana kuanzisha
vikundi mbalimbali vya ujasiriamali na kuvisajili ili waweze kupatiwa mikopo ya
asilimia 5% kwa vijana inayotolewa na Halmashauri za Wilaya kote nchini.
 
“Nawakumbusha kuwa tumeanzisha Mfuko
wa Elimu Wilaya ili kuboresha elimu katika Wilaya yetu kwa hiyo nawasihi vijana
wote kujitokeza kwenye kata zenu ili kushiriki shughuli ya ufyatuaji matofali
ambayo tumeelekeza kila Kata kufyatua matofali 10,000” Alisema Mtaturu
 
Mhe Mtaturu pia aliwasihi vijana kushiriki
kufanya kazi za kijamii ikiwa  ni  pamoja na kukagua utekelezaji wa
ilani ya CCM 2015-2020, kushiriki kuona shughuli mbali mbali za uzalishaji Mali
kupitia makundi ya vijana na kuwasaidia kwa kuwaunga mkono ili kuongeza
mtaji  wa miradi yao. 
Sambamba na hayo pia aliwatakia uchaguzi mwema wenye amani na utulivu, ambapo aliwasihi pindi watakapomaliza uchaguzi huo kuwa wamoja na kuvunja makundi ili kuendelea kuimarisha Jumuiya hiyo na Chama Cha Mapinduzi.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: DC MTATURU AWASIHI VIJANA KUDUMISHA NIDHAMU NA MSHIKAMANO
DC MTATURU AWASIHI VIJANA KUDUMISHA NIDHAMU NA MSHIKAMANO
https://1.bp.blogspot.com/-D5_C8trl4JE/WcgWxeky6aI/AAAAAAAAfOI/ahgOZggsNnwliXFr-sVt2FtpgtLxV9CGQCLcBGAs/s1600/1.JPG
https://1.bp.blogspot.com/-D5_C8trl4JE/WcgWxeky6aI/AAAAAAAAfOI/ahgOZggsNnwliXFr-sVt2FtpgtLxV9CGQCLcBGAs/s72-c/1.JPG
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/09/dc-mtaturu-awasihi-vijana-kudumisha.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/09/dc-mtaturu-awasihi-vijana-kudumisha.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy