DEREVA WA MBUNGE WA CHADEMA ASHAMBULIWA KWA MAPANGA

Dereva wa Mbunge wa Tarime Vijijini, John Wagesa Heche kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amevamiwa na kushambuliwa na mapanga usiku wa kuamkia leo akiwa mjini Tarime.
Dereva huyo anayejulikana kwa jina Suez Daniel Maradufu alivamiwa na watu hao waliokuwa na silaha majira ya saa mbili usiku Septemba 14 na kutokomea baada ya kumjeruhi.
Mbunge John Heche amethibitisha kutokea kwa tukio hilo baada ya kupata taarifa kutoka kwa Katibu wake, Mrimi Zablon ambaye amekiri kuwa dereva Suez ameshambuliwa na sasa yupo hospitali akipatiwa matibabu japo hali yake siyo nzuri.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post