DEREVA WA TUNDU LISSU ATOWEKA

Dereva wa Mbunge wa Singida Mashariki na Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), tundu Antipasi Lissu aliyepigwa risasi siku ya jumatano saa 7 mchana akitokea bungeni kwenda nyumbani kwake, ajulikanae kwa jina Adam anadaiwa kutoweka na kutokuonekana tangu siku ya tukio.
Akiongea na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto ameeleza kuwa tokea siku ya tukio hilo dereva huyo hajulikani alipo na wala hajaripoti kituo chochote cha Polisi ili kutoa maelezo kuhusiana na tukio la kufyatuliwa risasi kwa Lissu.
“Katika tukio hili, Mheshimiwa Tundu Lissu alikuwa na dereva anayefahamika kwa jina la Adam. Tokea tukio hili limetokea hatujamuona mpaka leo, sababu za kutokuonekana hazifahamiki….” alisema RPC Muroto.
“Natoa wito, natoa notisi kwa dereva Adam afike ofisi ya mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai Dodoma au afike ofisi ya mkurugenzi wa makosa ya jinai Dar es Salaam. Atupe taarifa zinazohusiana na tukio hili”.
“Sisi jeshi la Polisi tunaamini ni mtu muhimu na aliye na siri zinazohusiana na tukio hili,” aliongeza.
Vilevile alisema kuwa Jeshi la Polisi linamtaka Katibu Mkuu wa CHADEMA, Vicent Mashinji kufika katika ofisi ya mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai Dodoma au afike ofisi ya mkurugenzi wa makosa ya jinai Dar es Salaam ili aweze kutoa maelezo kuhusiana na anachokifahamu juu ya tukio hilo.
“Tunamtaka Mheshimiwa Vicent Mashinji ambaye ameonekana kwenye press conference Dar es Salaam ambae anasema yeye anawafahamu waliofanya hilo tukio afike Dodoma ofisi ya mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai  au afike ofisi ya mkurugenzi wa makosa ya jinai Dar es Salaam. Atupe chochote, atueleze kama watu wanafahamika waliofanya tukio yeye atoe maelezo kuhusiana na tukio hilo.” alisema.
Aidha RPC Muroto alitoa rai kuwa Jeshi la Polisi liachwe ili lifanye kazi yake ya uchunguzi na upelelezi bila kuingiliwa.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post