DK.SHEIN AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA LA CHAKULA NA KILIMO LA UMOJA WA MATAIFA (FAO)

Rais wa Zanzibar na Mweyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) Dkt.Jose Graziano da Silva alipofika Ikulu Mjini Unguja leo.
DSC_4658
Rais wa Zanzibar na Mweyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na mgeni wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) Dkt.Jose Graziano da Silva alipofika Ikulu Mjini Unguja leo,[Picha na Ikulu.] 07/09/2017.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amelipongeza Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) kwa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha sekta ya kilimo hapa nchini.

Dk. Shein aliyasema hayo leo Ikulu mjini Zanzibar wakati alipofanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Dk. Jose Graziano da Silva, ambaye amefika Zanzibar kwa lengo la kuongeza mashirikiano baina ya Shirika hilo na Zanzibar.

Katika mazungumzo hayo, Dk. Shein alimueleza Mkurugenzi Mkuu huyo kuwa FAO ni miongoni mwa Mashirika ya Umoja wa Mataifa yalio na historia kubwa katika kuisaidia Zanzibar katika sekta ya kilimo pamoja na mazao yanayohusiana na chakula.

Aliongeza kuwa FAO imeweza kutoa misaada mbali mbali ya kuendeleza sekta ya kilimo hapa Zanzibar na kumueleza Mkurugenzi Mkuu huyo jitihada za wananchi wa Zanzibar katika kuliendeleza zao la mwani na kusisitiza haja kwa Shirika hilo kuiunga mkono Zanzibar katika kuhakikisha kilimo hicho kinawanufaisha wakulima wake.

Pamoja na hayo, Dk. Shein alitoa pongezi za pekee kwa Shirika hilo kwa ushirikiano wake mkubwa unaotoa katika kupambana na athari za kilimo zinazosababishwa na wadudu waharibifu wa matunda ikiwa ni pamoja na utafiti wa maradhi ya zao la mwani.

Aidha, Dk. Shein alimueleza Mkurugenzi Mkuu huyo juhud
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post