JAJI MKUU ALIYEFUTA UCHAGUZI WA URAIS NCHINI KENYA ATUA TANZANIA

SHARE:

JAJI Mkuu wa Kenya, David Maraga ametua nchini katika mkutano wa majaji na mahakimu akionekana kivutio kwa wengine. Jaji huyo ni mmoja ...

JAJI Mkuu wa Kenya, David Maraga ametua nchini katika mkutano wa majaji na mahakimu akionekana kivutio kwa wengine.
Jaji huyo ni mmoja wa majaji wakuu 13 kutoka nchi mbalimbali duniani wanaohudhuria mkutano majaji na mahakimu wa nchi za Jumuiya ya Madola unaofanyika jijini Dar es Salaam kwa siku tatu..
Maraga amegeuka kivutio baada ya kushangiliwa na majaji waliohudhuria mkutano huo wakati alipotambulishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma.
Profesa Juma amempongeza Maraga kwa kuwakilisha mfano bora wa kulinda uhuru wa Mahakama kwa nchi nyingine duniani.
Kiongozi huyo ameonekana akiwa ameambatana na walinzi wanne ambao wanamfuata popote anapotembea nje ya mkutano huo.
Hata hivyo, Maraga amekataa kuzungumza na vyombo vya habari kwa madai amekuja kuhudhuria mkutano huo na siyo kwa jambo jingine lolote.
Mkutano huo umefunguliwa leo Jumatatu na Makamu wa Rais, Samia Suluhu ukiwa na kauli mbiu “Kujenga Mahakama Shirikishi, Thabiti na Inayowajibika.”
Jaji Maraga kwa siku za hivi karibuni amekuwa maarufu baada ya kutoa uamuzi wa kufuta Uchaguzi Mkuu wa Kenya uliokuwa umempa ushindi Rais Uhuru Kenyatta.
Katika mkutano huo Samia amesema rushwa ni kitu ambacho kinaondoa uhuru wa Mahakama na utawala wa sheria katika nchi mbalimbali duniani.
Samia amesema Tanzania inachukua hatua dhidi ya rushwa ili kuhakikisha kwamba Mahakama inatenda haki.
Amesema majaji na mahakimu wana wajibu mkubwa wa kuhakikisha Mahakama inakuwa uhuru kwa kuzingatia maadili ya kazi yao.
“Mahakama ya Tanzania itahakikisha kwamba rushwa haitakuwa sehemu ya utendaji wake. Tumetangaza vita dhidi ya rushwa katika ngazi zote za Serikali,” amesema Samia.
Kiongozi huyo wa Serikali amebainisha changamoto kubwa inayozikabili nchi mbalimbali duniani kuwa ni uhaba wa fedha za uendeshaji wa Mahakama, jambo ambalo linaathiri mifumo ya utoaji haki.
Kwa kutambua hilo, amesema Serikali inajitahidi kuongeza bajeti ya Mahakama kila mwaka wa fedha ili kesi ziamuliwe kwa haraka na kwa haki.
Kwa upande wake, Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma amesema bajeti ya Mahakama imeongezeka kwa asilimia 100 na wameanza kutekeleza mipango mbalimbali ya kuboresha utendaji.
Profesa Juma amefafanua kwamba katika mpango wa Taifa wa miaka mitano, Mahakama utakaokamilika 2020, zitajengwa mahakama 48 za wilaya, mahakama 100 za mwanzo na mahakama kuu 13 katika sehemu mbalimbali nchini.
“Bajeti inayokidhi mahitaji ni muhimu sana kwa uhuru wa mahakama. Tumekuwa na changamoto ya uhaba wa majengo ya mahakama lakini tunaendea kukabiliana nalo,” amesema.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: JAJI MKUU ALIYEFUTA UCHAGUZI WA URAIS NCHINI KENYA ATUA TANZANIA
JAJI MKUU ALIYEFUTA UCHAGUZI WA URAIS NCHINI KENYA ATUA TANZANIA
https://4.bp.blogspot.com/-4_l07_FActo/WclHXfB5V_I/AAAAAAAAfRc/W-yQFm9SKTAX4Ej6Xu-JiD6IRoFPohcwwCLcBGAs/s1600/justice-david-maraga-kenani.jpg
https://4.bp.blogspot.com/-4_l07_FActo/WclHXfB5V_I/AAAAAAAAfRc/W-yQFm9SKTAX4Ej6Xu-JiD6IRoFPohcwwCLcBGAs/s72-c/justice-david-maraga-kenani.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/09/jaji-mkuu-aliyefuta-uchaguzi-wa-urais.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/09/jaji-mkuu-aliyefuta-uchaguzi-wa-urais.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy