JINSI YA KUZINGATIA JAMBO MOJA

SHARE:

Ni kama kitu cha kawaida kwa siku za hivi karibuni kuona mtu akiwa anakula huku macho yake yote yakiwa kwenye simu, tv au kitu kingine to...

Ni kama kitu cha kawaida kwa siku za hivi karibuni kuona mtu akiwa anakula huku macho yake yote yakiwa kwenye simu, tv au kitu kingine tofauti. Hiki si kitu cha ajabu kwa siku hizi, japo naweza kusema limekua kama tatizo ambalo linawasumbua watu wengi.
Watu wengi kwa nyakati hizi wamekosa sana utulivu, wamekuwa ni watu wakutaka kufanya mambo mengi sana na kwa mkupuo. Kutokana na hili, ufanisi wa kazi umekuwa ukipungua na hakuna cha maana ambacho kimekuwa kikifanyika.
Kutokana na ujio wa teknolojia hasa ingizo la simu janja/ ‘smart phone’ hili limechangia sana kwa kiasi kikubwa kwa kuelekeza watu nguvu zao nyingi kwenye simu na kusahau majukumu ya msingi. Kwa mfano, ukiingia kwenye gari, ofisini au nyumbani ni rahisi kumkuta karibu kila mtu anatazama simu yake.
Lakini ukichunguza hata kile anachokitazama kinaweza kisiwe na maana sana, lakini ni hali ambayo ipo na inapelekea badala ya kufanya majukumu ya msingi, muda mwingi unakuwa unapotea kwenye simu na bila faida yoyote.
Nimekupa mfano kidogo ili upate picha ya kile ambacho nataka kusema. Simaanishi tu kwamba simu peke yake ndio imekuwa chanzo cha watu kufanya mambo kwa undumila kuwili, la hasha, bali watu wamekuwa na mambo mengi sana wao kama wao kutokana na kuibua tabia hii mpya.
Kwa sasa haishangazi tena kama mtu akianza jambo hili kabla hajamaliza anataka tena kurukia jambo lingine. Unaweza ukajiuliza kama akili haitulii sehemu moja, ukishika hiki unaacha na unakimbilia kitu kingine, sasa kwa mwendo huo ni kitu gani ambacho utaweza kweli kukifanikisha kwenye maisha yako?
Kwa kifupi hili ni tatizo na kwa wengi imekuwa ngumu sana kuweza kuvunja tabia hii kwa sababu ya mazoea, ingawa zipo mbinu au njia za kufanya hivyo. Kitendo cha kushindwa kuishinda hali hii, ni sawa na kuamua kuendelea kuharibu maisha yako.
Kwa vyovyote vile iwavyo, unatakiwa kujua jinsi utakavyoweza kuweka nguvu zako za uzingativu katika eneo moja ili uweze kutenda mambo yako kwa ufanisi na mafanikio. Itakuwa ngumu sana kwako kuweza kufanikiwa ikiwa utashindwa kuvunja tabia hii. Je, unawezaje hili;-
Hivi ndivyo jinsi unavyoweza kujifunza kuweka nguvu za uzingativu eneo moja.
1. Chagua jukumu moja la muhimu kutekeleza.
Asubuhi unapoamka mara baada ya kusali na kufanya ‘meditation,’ kabla hujawasha simu yako anza kutekeleza jukumu lako la muhimu. Najua unaweza ukawa una vitu vingi vya kufanya, lakini chagua kitu kiomoja tu cha kuanza nacho na vingine vyote visahau kwa muda mpaka ukamilishe jukumu lako moja la muhimu kwa wakati huo.
2. Jukumu ulilichagua lifanye kwa dakika 15 bila kuacha.
Katika dakika hizi usikubali kuingiliane na kitu chochote, tumia dakika hizo vizuri nguvu zako zote zihamishie hapo. Usichague dakika nyingi sana za kuanza kuweka nguvu za uzingativu kwa pamoja, anza kwanza na dakika chache, ikitokea umeshindwa dakika 15, punguza ziwe hata 10 au 5 lakini lazima uibuke mshindi.
3. Fanya kila siku na kwa kila kitu.
Ili tabia hii iweze kukaa na iwe yako, fanya kila siku na kwa kila kitu kiwekee nguvu ya uzingativu. Unapoamua kufanya kitu fulani mawazo yako yote hamishia hapo na bila shaka hapo utakuwa na ufanisi mwema wa kazi yako. Lakini ikiwa utashindwa zoezi hilo hiyo itakuwa ngumu kwa wewe kuweza kufanikiwa.
Inabidi ieleweke kwamba, kuweka nguvu za uzingativu katika eneo moja kwa masaa kadhaa, kwa siku kadhaa na kwa muda fulani maalumu kuna leta mabadiliko ya maisha yako bila kipangamizi chochote.
Ni jukumu lako leo kuanza kuweka nguvu zako za uzingativu kwa kila ukifanyacho ili kikuletee mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,

Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: JINSI YA KUZINGATIA JAMBO MOJA
JINSI YA KUZINGATIA JAMBO MOJA
https://2.bp.blogspot.com/-61bbwogSpuA/Wcgq18vsbiI/AAAAAAAAfO4/BKRGkwc_yUQa7A7n8yyhR_zKMw7-qLD9wCLcBGAs/s1600/hqdefault.jpg
https://2.bp.blogspot.com/-61bbwogSpuA/Wcgq18vsbiI/AAAAAAAAfO4/BKRGkwc_yUQa7A7n8yyhR_zKMw7-qLD9wCLcBGAs/s72-c/hqdefault.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/09/jinsi-ya-kuzingatia-jambo-moja.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/09/jinsi-ya-kuzingatia-jambo-moja.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy