KIBA KUAMSHA TIGO FIESTA ARUSHA

Staa wa Ngoma ya Seduce Me, Ali Kiba.
MKALI wa Ngoma ya Seduce Me, Ali Kiba, anatarajiwa kuwa miongoni mwa kundi la wasanii wa muziki watakaoangusha burudani Jumamosi hii (Septemba 9) katika Tamasha la Tigo Fiesta ndani ya Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.
Akizungumza na Over Ze Weekend, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo ambao ndiyo wadhamini wa tamasha hilo, William Mpinga amesema tayari wanamuziki zaidi ya 17 akiwemo Kiba wameshasajiliwa kwa ajili ya kutoa burudani katika Tigo Fiesta ambayo itafanyika mikoa mbalimbali.
“Hadi sasa wasanii zaidi ya 17 akiwemo Kiba, Christian Bella, Shilole, John Makini, Mr. Blue, Saida Karoli na wengine wameshasajiliwa, huu ni muda wenu wapenzi wa burudani kukata tiketi mapema kwa njia ya Tigo Pesa kupitia namba 0678888888 ambapo litatokea jina la Tigo Fiesta na atakayefanya muamala huo atapatiwa tiketi yake kwenye maduka ya tigo mkoa linapofanyika tamasha,” alisema Mpinga na kuongeza kuwa kwa mteja atakayenunua tiketi kwa njia hiyo atapata punguzo la asilimia 10.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post