KIMBUNGA IRMA CHAZIDI KULETA MAAFA HUKU WATU MILIONI 6.3 WAKITAKIWA KUHAMA NYUMBA ZAO

Kimbunga kiitwacho Irma kimelikumba eneo la Florida huku kikiwa na upepo wenye mwendo wa kasi ya Kilomita 209 kwa saa.

Kimbunga hicho ambacho kimeshauwa watu watatu Florida kimepandishwa daraja na kufikia daraja la 4 kwa ukubwa.

Watu milioni 6.3 wameshambiwa kuondoka kwenye nyumba zao kwa lazima ama kwa hiyari yao ili kuepuka maafa.

Kimbunga hicho tayari kimesababisha vifo vya watu 25 katika eneo la ukanda wa Caribbean tangu kilipoanza mapema wiki hii.
                                              Boti likiwa limesukumwa kando na kimbunga Irma
                                  Kimbunga Irma kikiwa kimeuangusha mti ulioangukia gari 
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post