MAAGIZO YA RAIS MAGUFULI BAADA YA TUNDU LISSU KUSHAMBULIWA KWA RISASI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amezungumzia tukio la kushambuliwa kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu akisema kuwa amesikitishwa na amepokea kwa masononeko makubwa tukio hilo.
“Nimepokea kwa masikitiko tukio la kupigwa risasi Mh.Tundu Lissu, namuombea kwa Mwenyezi Mungu aweze kupona haraka. “
Aidha, Rais Magufuli ambaye ndiye Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ameviagiza vyombo vya usalama kuhakikisha wanawasaka, wanawakamata na kuwafikisha wahusika katika vyombo husika ili sheria iweze kuchukua mkondo wake kufuatia tukio hilo la kinyama.
“Aidha, vyombo vya dola viwasake wale wote waliohusika na tukio hili la kinyama na kuwafikisha ktk mikono ya sheria.”
Mbali na Rais Magufuli, viongozi mbalimbali wa serikali, wabunge na watanzania mbalimbali, wametuma salamu zao za pole kwa familia ya Tundu Lissu kufuatia tukio hilo lililotokea leo mchana mkoani Dodoma.
Tundu Lissu amejeruhiwa kwa risasi maeneo ya tumboni na mguu baada ya gari lake kushambuliwa wakati alipokuwa akitokea bungeni kwenda nyumbani kwake eneo la Area D.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post