Maana za taa zinazowaka katika dashbodi ya gari

SHARE:

Wakati jambo ambalo si sahihi linatokea kwenye gari lako mfumo wa umeme uliopo kwenye gari hutoa ishara kwenye dashibodi kwa kuwasha taa amb...Wakati jambo ambalo si sahihi linatokea kwenye gari lako mfumo wa umeme uliopo kwenye gari hutoa ishara kwenye dashibodi kwa kuwasha taa ambayo itaashiria kuwa kuna tatizo sehemu fulani.

Kuna baadhi ya ishara zinapotokea, unatakiwa kurekebisha kabla ya kuendelea na safari kwa ajili ya usalama wako wakati ishara nyingine zikitokeo unaweza kuendelea na safari na ukazirekebisha muda utakaopenda wewe, lakini ni muhimu kuzirekebisha.

Wakati mwingine ishara hizi zinaweza kuwa tofauti kulingana na gari pamoja na nchi ambayo gari hilo limetengenezwa, lakini unapopata changamoto kutambua ishara inayoonyeshwa kwenye dashibodi, wasiliana na mtaalamu au soma kitabu cha muongozo wa namna ya kulitumia hilo gari (Users manual).

1. Ishara ya kupanda kwa joto la injini.Ishara hii inaonyesha kuwa injini ya gari lako imepata joto sana na unatakiwa kuchukua hatua kadhaa kuhakikisha inarudi kwenye hali yake ikiwemo kulizima gari na kuliacha kwa muda ili lipoe.

Miongoni mwa mambo yanayosababisha injini kupata joto zaidi kipoozeo (coolant) kwenye rejeta kupungua sana au kumaliza muda wa matumizi, au uwepo wa tatizo katika mfumo wa kilainishi cha injini (engine oil).

Hatua za awali unazoshauri kufanya injini ikipata joto kupitiliza ni kuzima vitu ambavyo sio muhimu sana kama redio, kiyoyozi ili kuipunguzia injini mzigo. Pia unashauriwa kuegesha gari lako sehemu tulivu, na usifungue rejeta hadi dakika 30 zipite kwani kama imepata moto sana inaweza kurusha kipoozeo (coolant) na kukusababishia majeraha.

Baada ya hatua hizo unaweza kuwasiliana na mtaalamu kwa hatua zaidi.

2. Tahadhari ya upepo wa tairiIshara hii inaonyesha kuwa, upepo katika moja au baadhi ya tairi za gari lako zinaupepo pungufu na kwamba unatakiwa kuongeza kabla ya kuanza safari au kuendelea na safari.

Kikubwa cha kuzingatia hapa ni kuwa, kila tairi ina kiwango cha upepo inachoweza kuhimili, hivyo ni muhimu kufahamu kiwango cha upepo wa tairi ya gari lako. Mara nyingi, tairi za nyuma za gari huwekwa upepo mwingi kuliko za mbele.

3. Tahadhari wa mafuta ya injini (engine oil)Alama hii inaashiria kwamba mafuta ya injini yamebaki kidogo hivyo unatakiwa kuongeza ama kuna tatizo katika msukumo wa mafuta ya injini.

Kazi kubwa ya mafuta ya injini ni kulainisha vyuma ndani ya injini kuepusha visisuguane lakini pia kuvilinda visipate kutu.

4. Ishara ya utelezi (traction control)Taa hii huwaka baada ya dereva kubonyeza kitufe ambacho kitaisaidia gari kutoyumba linapopita katika eneo lenye utelezi.

5. Tahadhari ya Injini (engine malfunction)Taa ya injini kwenye dashibodi ya gari lako huwaka kwa kusababishwa na mambo mbalimbali ikiwemo kulegea kwa mfuniko wa tenki la mafuta, kuna tatizo katika plagi za gari lako au nyaya za plagi, kifaa kinachopima kiwango cha upepo unaoingia kwenye injini kinahitaji kubadilishwa.

Sababu nyingine ni kuwa kifanyaa kinachobadilisha gesi ya carbon monoxide kuwa carbon dioxide kimeharibika, au kitambuzi cha Oksijeni ambacho hupima kiwango cha oksijeni ambayo haijatumika katika injini kina matatizo.

6. Breki ya gari (ABS)‘Anti-lock Brake System’ (ABS) ni mfumo kwenye breki ya gari ambayo huzuia breki kusimamisha gari kwa ghafla hata kama utakanyaga breki ghafla. Hii imewekwa ili kuzuia gari kupinduka kwani gari likiwa kwenye mwendo ukakanyaga breki ghafla, lingekuwa halina ABS uwezo wake wa kupinduka ni mkubwa sana.

Taa hii inapowaka inaashiria kuwa kuna tatizo kwenye ABS na ni vyema likashughulikiwa haraka kuweza kuepuka madhara zaidi.

7. Tahadhari ya kuwasha injiniIshara hii humaanisha kuwa unahitaji kukanyaga breki ya gari ili uweze kuliwasha au kuhamisha kutoka ‘neutral’ kuweka gia tayari kuanza mwendo. Mara nyingi hii huwepo katika magari ya automatiki.

8. Betri ya gariTaa hii huwaka kuashiria kuwa chaji ya betri ya gari lako imepungua sana na kwamba huenda kuna tatizo katika mfumo wa kuchaji betri.

Unatakiwa kujua kama tatizo ni betri au gari ili ujue ni kitu gani utakirekebisha.

9. MafutaAlama hii hukuashiria kuwa kiwango cha mafuta kwenye gari lako kimepungua. Lakini hii haimaanishi kuwa gari litazima muda huo, unaweza kwenda hadi kilomita 20 kabla gari lako halijazima. Ila ni vyema ukaongeza mafuta pale taa inapowaka ili kuepusha kuzima kwa gari kwani kunaweza kusababisha uchafu ulioko kwenye tenki kuingia katika mfumo wa injini na kusababisha madhara zaidi.

Pembeni ya taa ya mafuta, kuna mshale ambao huonyesha upande ambao tenki la mafuta lipo.

10. Kufunga mkandaUnapowasha gari lako na kuanza safari, kama hujafunga mkanda, taa hii huwaka kukutaka ufanye hivyo kwani ni kwa usalama wako binafsi. Katika magari ya kisasa, alamu hulia hadi pale wewe dereva na abiria aliyekaa katika kiti cha mbele mtakapofunga mikanda.

11. Fuko la hewa (Air bags)Mfuko wa hewa (airbag) huchomoza mbele yako kwa haraka pale unapopata ajali ya kugonga kitu ili kukuzuia usijigonge sehemu nyingine ya gari na kuumia zaidi.

Kuwaka kwa taa hii husababishwa na kuwepo kwa tatizo katika moja au zaidi ya fuko la hewa, au tatizo katika mfumo wa fuko hilo.

Inakubidi kuhakikisha kuwa unaligundua tatizo na kurekebisha haraka kwa ajili ya usalama wako na abiria uliowabeba ndani ya gari.

12. Taa za ukungu (fog lights)Ishara hii huonyesha kuwa taa za gari zinazotumika endapo kuna ukungu zinawaka. Hii utakusaidia kujua kama huzihitaji uzizime.

Taa hizi hutumika kukiwa na ukungu ili madereva wengine au watumiaji wengine wa barabara waweze kuona gari lako.

13. Taa ya ulinziMagari mengi yana mfumo wa ulinzi ambapo hutoa sauti au ishara fulani punde kinapofanyika kitu ambacho si cha kawaida, mfano mtikisoko mkubwa au kugongwa.

Taa hii inapowaka inaashiria kuwa, kuna tatizo katika mfumo wa ulinzi wa gari lako, hivyo ni vyema ukachukua hatua za haraka ili kuhakikisha gari linakuwa salama.

14. UteleziTaa hii hutoa ishara kwamba kuna tatizo katika mfumo wa kuzuia gari kuteleleza linapopita katika eneo lenye utelezi, na kwamba huenda mfumo huo umezima kabisa.

15. Maji ya wiperIshara hii huonyesha kuwa maji ya kiosheo (wiper) cha vioo vya gari yapo chini, unatakiwa kuyaongeza ili kuweza kuhakikisha vioo vya gari lako vinakuwa safi.

Zipo ishara nyingi zaidi ya hizi, na ili kuwa salama unapoendesha gari, hakikisha unazifahamu vizuri ili kuepuka kuharibikiwa na gari uwapo safarini.

Pia, alama hizo zinaweza zikatofautiana wa kiasi kulingana na magari, lakini nyingi hufanana.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: Maana za taa zinazowaka katika dashbodi ya gari
Maana za taa zinazowaka katika dashbodi ya gari
http://zotekaliblog.com/wp-content/uploads/2017/09/banner-750x375.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/09/maana-za-taa-zinazowaka-katika-dashbodi.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/09/maana-za-taa-zinazowaka-katika-dashbodi.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy