MABASI YA MWENDOKASI YAANZISHA SAFARI MBILI MPYA DAR ES SALAAM

Katika hali ya kuhakikisha kuwa wanaboresha usafiri na kuvutia abiria wengi katika jiji la Dar es Salaam, waendeshaji wa mradi wa mabasi ya mwendokasi (UDART) wamenzisha safari mpya za mabasi hayo zitakazoanza kutumika Septemba 4 mwaka huu.
Akizjngumza na gazeti la The Citizen kwa njia ya simu, Afisa Uhusiano wa UDART, Deus Buganywa alisema kuwa safari hizo za Morocco hadi Ubungo na Ubungo hadi kimara zitaanza kesho.
Buganjwa alisema kuwa mabadiliko yatahusisha pia safari za Jumatatu hadi Ijumaa ambapo mabasi yenye namba 007 (route 7) yanayosafirisha abiria kutoka Kimara hadi Morocco yatakuwa yakitoa huduma kuanzia saa 11:00 asubuhi hadi saa 4:00 usiku.
Katika safari mpya zilizoanzishwa, mabasi yenye namba 008 (route 8) yatakuwa yakisafirisha abiria kutoka Morocco hadi Kituo cha Mabasi Ubungo.
Aidha, afisa huyo alisema kuwa, mabasi yenye namba 009 (route 9) yatakuwa yakisafirisha abiria kutoka Kituo cha Mabasi Ubungo hadi Kimara.
Buganywa alisema hili ni suluhusisho la muda kuhakikisha kuwa abiria hatumii zaidi ya dakika nne katika kituo akisubiria basi.
Alithibitisha kuwa kampuni hiyo ina mpango wa kununua mabasi mengine mapya katika kile walichoeleza kuwa ni kuhakikisha kwamba wanaboresha huduma ya usafiri jijini Dar es Salaam.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post