Madhara ya unywaji pombe kwa mama mjamzito

SHARE:

Mtoto awapo tumboni hupata chakula (maji na virutubisho lishe) vyote kupitia kwa mama yake. Mama akila mlo ulio kamili awapo mja mzito mtoto...

Mtoto awapo tumboni hupata chakula (maji na virutubisho lishe) vyote kupitia kwa mama yake. Mama akila mlo ulio kamili awapo mja mzito mtoto pia hupata mlo kamili na iwapo mama hapati mlo kamili huwa hivyo kwa mtoto pia. Je mtoto anakulaje awapo tumboni? Chakula huingia mwilini kwa mtoto anayekuwa tumboni mwa mama yake kupitia kondo la nyuma au ‘placenta’ kwa Kiingereza. Hivyo mama anywapo pombe vilevile nayo huingia kwa mtoto kupitia kondo la nyuma.Pombe hujipenyeza kwa kasi katika kondo la nyuma la mama na kiwango cha kilevi katika mwili wa mtoto (blood alcohol level) huwa sawa na kiwango cha pombe kilichomo katika mwili wa mama. Kwamba humuoni mtoto awapo tumboni si hoja sana kwani ushahidi unaonyesha kwamba athari za unywaji pombe wa mama una matokeo hasi katika ukuaji wa mtoto. Yaani baadhi ya athari huwa na matokeo ya kudumu ikiwa ni pamoja na kudumaa kwa akili za mtoto pindi anapozaliwa, madhara ya jumla katika ukuaji wa mwili hasaa ubongo wa mtoto.

Iwapo ulikunywa pombe ukiwa mjamzito, je ni zipi dalili za athari za pombe kwa mtoto? Ingawa dalili ni nyingi, makala haya yatajikita katika dalili za kudumaa kwa akili ya mtoto baada ya kuzaliwa. Mtoto mwenye tatizo hili hupata taabu kuwakumbuka ndugu na jamaa wa karibu hata wale anaoshinda nao nyumbani.

Ingawa watoto wa umri huu hupendelea kucheza na vitu vinavyowazunguka, mtoto huyu hapendi ‘kujishughulisha’ na vitu vinavyomzunguka. Unashauriwa kumpeleka mtoto kwa wataalamu wa afya kupata msaada zaidi pindi unapohisi mtoto ana tatizo.

Mwongozo wa kitaalamu wa makuzi ya mtoto unaonesha kwamba mtoto wa umri wa miezi sita anapaswa kuwa na uwezo wa kufanya mengi ya mambo yafuatayo; toka anazaliwa anapaswa kuweza kugeuza shingo lake kufuata mwelekeo sauti inakotokea, aweze kushika miguu yake akiwa amelala kifudifudi, aweze kukuangalia anapokuwa ananyonya / kula, aweze kutabasamu aonapo nyuso na kusikia sauti za watu anaowafahamu, aweze kulia anapoudhiwa / ama akiwa hajisikii vizuri (mgonjwa, njaa, nk.), apate kutoa sauti mbalimbali ikiwapo kwikwi ndogondogo na hata kupiga kelele na mwisho awe na tabia ya kutaka kutia kila akishikacho mdomoni mwake.

Moja ya njia kuu za kumlinda mtoto na madhara yatokanayo na unywaji pombe ni kwako mama mjamzito kuacha kunywa pombe mara tu unapogundua una ujauzito. Iwapo huwezi kabisa kuacha kunywa pombe basi unashauriwa kwenda kwa daktari na kupata ushauri zaidi. Kumbuka kuacha kunywa pombe katika hatua yoyote ya ujauzito kutakuongezea nafasi ya kujifungua mtoto mwenye afya na siha njema.

Chanzo: Mwananchi

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: Madhara ya unywaji pombe kwa mama mjamzito
Madhara ya unywaji pombe kwa mama mjamzito
http://bongo5.com/wp-content/uploads/2017/09/drink_2779990b.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/09/madhara-ya-unywaji-pombe-kwa-mama.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/09/madhara-ya-unywaji-pombe-kwa-mama.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy