MAKUBALIANO YA KUWAREJESHA NYUMBANI WAKIMBIZI WA BURUNDI YATIWA SAINI

SHARE:

Tanzania, Burundi na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wakimbizi (UNHCR) wamepitisha mpangokazi wa kuwarejesha nyumbani wakim...

Tanzania, Burundi na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wakimbizi (UNHCR) wamepitisha mpangokazi wa kuwarejesha nyumbani wakimbizi raia wa Burundi ambao tayari wamejiandikisha kwa hiari kurejea nyumbani.
Mpangokazi huo ni sehemu ya makubaliano yaliyotiwa saini leo kufuatia Kikao cha 19 cha Kamisheni ya Pande Tatu kilichofanyika jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na mawaziri wanaoshughulikia wakimbizi wa Tanzania, Burundi na mwakilishi wa UNHCR.
Chini ya Mpangokazi huo wa kipindi cha karibu miezi minne (07 Septemba hadi 31 Disemba, 2017) wakimbizi 12,000 ambao tayari wamejiandikisha kwa hiari watarejeshwa nyumbani huku ukitoa nafasi kwa wengine zaidi watakaojiandikisha kujumishwa.
Makubaliano hayo yalitiwa saini na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba, Waziri wa Mambo ya Ndani na Elimu ya Uzalendo wa Burundi Pascal Barandagiye na Mwakilishi wa UNHCR nchini Bibi Chansa Ruth Kapaya.
Chini ya Makubaliano hayo shirika la UNHCR na washirika wake wataweza kutembelea maeneo ya mipakani ya Tanzania na Burundi kwa lengo la kusaidia mchakato wa urejeshaji wa hiari wa wakimbizi hao na masuala mengine yanayohusu hifadhi ya wakimbizi na raia wengine wanaohitaji hifadhi.
Pande hizo za makubaliano zimetoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kutoa ushirikiano katika kutekeleza zoezi la kuwarejesha nyumbani wakimbizi hao na kulitaka shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) kutoa chakula kwa wakimbizi wanaorejea kwa kipindi cha miezi mitatu.
Kikao hicho cha 19 cha Kamisheni ya Pande Tatu kimeeleza kutumbua na kuthamini ukarimu wa watanzania ambao umewezesha mamilioni ya wakimbizi kuishi Tanzania tangu nchi hiyo ilipopata uhuru mwaka 1961 na zaidi kuendelea kuwakarimu wakimbizi wapatao 350,000 miongoni mwao 256,850 wakiwa raia wa Burundi.
1Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwigulu Nchemba (Katikati), akisaini hati ya makubaliano ya kuwarejesha makwao wakimbizi  wa Burundi waishio Tanzania wakati wa mkutano wa siku moja uliofanyika leo Jijini Dar es Salaa. Kutoka kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani wa Burundi Bw. Pascal Barandagiye, Mkurugenzi wa Huduma za Wakimbizi Tanzania Bw. Harrison Mseke, Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi nchini Tanzania (UNHCR), Bi. Chansa Ruth Kapaya na Mwakilishi wa  Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi nchini Burundi Bw. Abel Mbilinyi.
2Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwigulu Nchemba akibadilisha hati ya makubaliano ya kuwarejesha makwao Wakimbizi kutoka Burundi waishio Tanzania na  Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi nchini Tanzania (UNHCR), Bi. Chansa Ruth Kapaya katika mkutano wa siku moja uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
3
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwigulu Nchemba akimsikiliza Mkurugenzi wa Huduma za Wakimbizi Tanzania Bw. Harrison Mseke baada ya kusaini hati za makubaliano ya kuwarejesha makwao wakimbizi  wa Burundi waishio nchini Tanzania katika mkutano wa siku moja majadiliano kuhusu urejeshwaji wa wakimbizi hao uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
4
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwigulu Nchemba (katikati) akiteta jambo na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi nchini Tanzania (UNHCR) Bi. Chansa Ruth Kapaya, kulia  ni Mwakilishi wa  Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi nchini Burundi (UNHCR) Bw. Abel Mbilinyi na kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani wa Burundi Bw. Pascal Barandagiye na Mkurugenzi wa Huduma za Wakimbizi Tanzania Bw. Harrison Mseke (wapili kushoto) wakati wa mkutano wa  siku moja wa kusaini makubaliano ya kuwarejesha makwao wakimbizi kutoka Burundi waishio nchini Tanzania leo Jijini Dar es Salaam.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: MAKUBALIANO YA KUWAREJESHA NYUMBANI WAKIMBIZI WA BURUNDI YATIWA SAINI
MAKUBALIANO YA KUWAREJESHA NYUMBANI WAKIMBIZI WA BURUNDI YATIWA SAINI
https://3.bp.blogspot.com/-GDoFMz2vGDM/WakJAT6ILWI/AAAAAAAAeOo/aS6gy8k5lEY3J8Iti3-rRIto0QTZrsQNACLcBGAs/s1600/x1-147-750x375.jpg.pagespeed.ic.wGxXpm8l-q.webp
https://3.bp.blogspot.com/-GDoFMz2vGDM/WakJAT6ILWI/AAAAAAAAeOo/aS6gy8k5lEY3J8Iti3-rRIto0QTZrsQNACLcBGAs/s72-c/x1-147-750x375.jpg.pagespeed.ic.wGxXpm8l-q.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/09/makubaliano-ya-kuwarejesha-nyumbani.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/09/makubaliano-ya-kuwarejesha-nyumbani.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy