MANCHESTER UNITED YAANZA NA USHINDI LIGI YA MABINGWA ULAYA

Timu ya Manchester United imerejea katika Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa ushindi waliostahili wa magoli 3-0 dhidi ya timu ya Uswizi ya Basel.

Marouane Fellaini, aliyeingia kuchukua nafasi ya Paul Pogba aliyeumia katika kipindi cha kwanza, aliruka juu na kufunga goli la kwanza kwa kichwa mpira uliopigwa na Ashley Young.

Romelu Lukaku aliongeza goli la pili akiwa katika msitu wa wachezaji wa Basel baada ya kunasa krosi ya Daley Blind, Marcus Rashford akafunga la tatu dakika saba tu tangu aingie dimbani.
       Marouane Fellaini akiruka juu na kuupiga kwa kichwa mpira uliozaa goli la kwanza
                     Romelu Lukaku akijipinda kujaribu kufunga goli katika mchezo huo 
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post