MANENO ALIYOSEMA TUNDU LISSU BAADA KUPATA FAHAMU HOSPITALINI

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu anayepatiwa matibabu katika Hospitali ya Aga Khan jijini Nairobi amemtaka Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kuendeleza mapambano ambayo tayari wameyaanza.
Tundu Lissu ambaye anapatiwa matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi jijini Dodoma eneo la Area D nyumbani kwake na watu wasiojulikana aliyesema hayo jana baada ya kupata fahamu akiwa hospitalini.
Katika ujumbe uliowekwa kwenye ukurasa wa Twitter wa Mbunge wa CHADEMA Iringa Mjini, Peter Msigwa ambaye naye yupo jijini Nairobi alisema  Lissu alisema alipona ili kuja kusimulia tukio hilo na kumtaka Mbowe kuendeleza mapambano.
“Mwenyekiti I survived to tell the tale. Please keep up the fight,” ni maneno machache aliyosema Lissu jioni hii (jana) baada ya kufumbua kinywa, alisema Msigwa.
Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi linaendelea na msako wa kuwakamata watu wote waliohusika katika tukio hilo ambapo hadi sasa magari manane aina ya Nissan Patrol yamekamatwa kwa ajili ya uchunguzi.
Aidha, Polisi wamesema kuwa wanamhitaji Dereva wa Tundu Lissu na Katibu Mkuu wa CHADEMA kwa ajili ya mahojiano kuhusiana na tukio hilo.
Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi Alhamisi, Septemba 7 mwaka huu wakati akitokea bungeni kwenda nyumbani kwake.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post