MAOMBI YA TUNDU LISSU YAWAPELEKA WATANO RUMANDE

Watu watano wanashikiliwa na jeshi la Polisi baada ya kufika katika viwanja vua TIP vilivyopo Sinza, Dar es Salaam kwa ajili ya kumuombea Tundu Lissu aliyeko hospitali jijini Nairobi akitibiwa majeraha aliyoyapata kutokana na shambulizi la risasi.
Akizungumza uwanjani hapo Jumapili ya leo Septemba 17, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Muliro Jumanne Muliro ameeleza kuwa Jeshi la Polisi haliyofumbia macho kuona matendo ya uvunjifu wa Amani yakitokea katika na badala yake litahakikisha usalama wa raia na mali zao.
“Wale wenye nia mbaya ambao bila shaka wana agenda binafsi zenye uelekeo wa kutishia maswala ya kiimani, mimi kaka Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni siwezi kukubali hali hiyo ikatoke kwenye eneo langu” alisema Kamanda Muliro.
Mapema siku ya Ijumaa Septemba 15 mwaka huu Jeshi la Polisi liliwaonya Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) kutoshiriki maandamano waliyokuwa wameyapanga kufanya katika viwanja hivyo siku ya leo.
Hata hivyo siku ya Jana Jumamosi Septemba 16 Mwenyekiti wa BAVICHA alitangaza kuwepo kwa mkusanyiko huo wa maombi na siyo maandamano kama walivyoyataja Polisi.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post