Nape amaeulizwa na wanakjijiji Bombardier inasaidia nini?

SHARE:

Wananchi wa jimbo la Mtama mkoani Lindi wamemhoji mbunge wao, Nape Nnauye kuhusu ndege aina ya Bombardier, wakitaka kujua inawasaidiaje. N...

Wananchi wa jimbo la Mtama mkoani Lindi wamemhoji mbunge wao, Nape Nnauye kuhusu ndege aina ya Bombardier, wakitaka kujua inawasaidiaje.
Ndege mbili aina ya Bombardier Dash 8 Q400 zilinunuliwa na Serikali kwa ajili ya kulifufua shirika la usafiri wa anga la Air Tanzania (ATCL), ambalo lilikuwa limezorota na kutishia uhai wake.
Ndege hizo zilizinduliwa na Rais John Magufuli Septemba 28, 2016 jijini Dar es Salaam.
Lakini wananchi wa Mtama bado hawajaona umuhimu wake na walimuhoji Nape, ambaye alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Jana Nape aliandika katika akaunti yake ya Twitter kuhusu utashi huo wa wananchi wake kuhusu Bombardier.
“Watu hawa wanapambana na hali zao! Waliniuliza bombardier ndiyo nini” na sie wa vijijini tutafaidikaje au ni kwenu mjini tu!?” ameandika Nape katika akaunti hiyo.
Alipoulizwa kwa njia ya simu na gazeti hili, Nape aliyewahi kuwa katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, alithibitisha kutuma ujumbe huo, akisema ni swali aliloulizwa na wanakijiji.
“Mimi sijui kwa nini mnauliza sana hicho kitu,” alisema alipozungumza na Mwananchi jana jioni.
“Mimi nilikuwa jimboni kwangu nazungumza na wananchi kuhusu korosho, mwanakijiji mmoja akauliza kwamba hiyo Bombardier ina faida gani? Na mimi nimeripoti maneno yake. Si maneno yangu.
“Suala si mimi kuwa na cheo, mimi ni mbunge wa wananchi. Hilo swali hata wewe ukiliuliza hapo mtaani utapata majibu matano tofauti.
“Nilikuwa nazungumza na wanavijiji kuhusu fedha zinazotolewa na Serikali kuhusu korosho, mbaazi na mazao mengine, ndipo nikaulizwa na mimi nimeripoti kwa rafiki zangu nilivyoulizwa.”
Lindi na Mtwara ni kati ya mikoa iliyokuwa inafikika kwa shida kabla ya Serikali kujenga barabara zilizorahisisha usafiri. Pamoja na usafiri wa barabara, Air Tanzania imeanzisha usafiri wa anga kwa ajili ya kuhudumia wasafiri wengine kwenda na kutoka mikoa hiyo ambayo hivi sasa inachangamshwa na uwekezaji katika gesi na viwanda vya saruji.[/caption]

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: Nape amaeulizwa na wanakjijiji Bombardier inasaidia nini?
Nape amaeulizwa na wanakjijiji Bombardier inasaidia nini?
http://zotekaliblog.com/wp-content/uploads/2017/09/air-tanzania-q400.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/09/nape-amaeulizwa-na-wanakjijiji.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/09/nape-amaeulizwa-na-wanakjijiji.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy