NASSARI AANIKA MAZITO MADIWANI CHADEMA WALIOPOKELEWA NA JPM

SHARE:

Mbunge wa Chadema wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari akiwahutubia wananchi. MBUNGE wa Chadema wa Arumeru Mashariki, Joshua Nass...

Mbunge wa Chadema wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari akiwahutubia wananchi.
MBUNGE wa Chadema wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari ameweka rehani ubunge wake  baada ya Rais John Magufuli kumpokea aliyekuwa diwani wa chama hicho aliyejiuzulu akisema ni kwa sababu ya kuunga mkono juhudi za Rais.
Nassari aliyasema hayo jana Jumapili na kudai ana ushahidi wa kielektroniki unaoonyesha madiwani hao walivyopewa rushwa ili wajiuzulu nafasi zao.
Hata hivyo, diwani wa Kata ya Kimandolu, Mchungaji Rayson Ngowi ambaye amepokewa na Rais Magufuli juzi  baada ya kujiuzulu Chadema akizungumzia tuhuma hizo alisema madai hayo hayana ukweli wowote na kama Nassari ana ushahidi ni vyema angeutoa hadharani.
Ngowi aliwashauri Chadema mkoani Arusha watatue matatizo yaliyopo ndani ya chama hicho na wasitafute visingizio kwa kuwa yeye ameamua kujiuzulu kwa kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli na hajapewa rushwa yoyote.
Diwani mwingine aliyejiengua katika chama hicho wa Kata ya Muriet, Credo Kifukwe alisema hakuna chochote alichopewa kama rushwa kwa lengo la kujiuzulu, akimshauri Nassari autoe hadharani ushahidi anaousema na si kushusha tuhuma zisizo na mashiko.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Arusha, Nassari alisema ushahidi huo ameuhifadhi ndani ya ‘flash disc’ na yuko tayari kumkabidhi Rais Magufuli na vyombo vya uchunguzi.
Mbunge huyo alisema endapo ikithibitika kuwa ushahidi wake ni wa uongo yuko tayari kujiuzulu nafasi yake ya ubunge.
“Ninao ushahidi na kama Mheshimiwa Rais yuko tayari niko tayari kumpatia ninayo flash, ushahidi ninao kwa muda mrefu na tulijua watapokelewa juzi madiwani wawili lakini mmoja amekataa akaenda mmoja,” alisema Nassari. 
 
Alidai kwamba  kwa kipindi kirefu alipokuwa masomoni nchini Uingereza alikuwa akijiuliza ni kwa nini madiwani katika Mkoa wa Arusha wamekuwa wakijiuzulu na ndipo alipoamua kufanya uchunguzi wa kina.
Nassari akiwa ameambatana na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema katika mkutano huo, alisema alianza kufanya uchunguzi Mei kwa kutumia vifaa vya kielektroniki alivyovinunua nchini Uingereza na kubaini kwamba baadhi ya madiwani wanaojiuzulu walipewa rushwa ya fedha, ahadi ya vyeo na ya makazi.
Alisema uchunguzi juu ya tuhuma za madiwani hao kujiuzulu aliufanyia ndani ya ofisi ya umma akisisitiza hakuna diwani wa Chadema mkoani Arusha ambaye amejiuzulu kwa kumuunga mkono Rais Magufuli bali wamepewa rushwa.
“Mheshimiwa Rais anapambana na rushwa lakini kuondoka kwa madiwani ni mfumo wa rushwa anaopambana nao niko tayari kujiuzulu nafasi yangu ya ubunge endapo ikithibitika ushahidi wangu ni wa uongo,” alisema Nassari.
Madiwani wapatao 10 wa Chadema wamejiuzulu kwa nyakati tofauti. Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole ameshawahi kunukuliwa akikanusha tuhuma za kupewa rushwa madiwani wanaojiengua kutoka Chadema na kujiunga na CCM.
Polepole Julai alikaririwa akisema iwapo Chadema ina viongozi wanaoweza kuhongwa na wakahongeka basi ni chama cha  ovyo kwa kuwa chama kilicho imara na watu wake wapo safi hawawezi kuhongeka.
Alitoa kauli hiyo mjini Bagamoyo alipohudhuria mahafali ya Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu (Tahliso) Mkoa wa Pwani.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,73,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,273,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,13,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,567,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3301,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,333,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,386,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,68,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1379,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1286,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: NASSARI AANIKA MAZITO MADIWANI CHADEMA WALIOPOKELEWA NA JPM
NASSARI AANIKA MAZITO MADIWANI CHADEMA WALIOPOKELEWA NA JPM
https://2.bp.blogspot.com/-oYHqzPtTTlk/Wci8Bvm1e9I/AAAAAAAAfP8/_fyB0vD-9QAoDyzwyTzA3fHOHgEIqebFgCLcBGAs/s1600/nassari.jpg
https://2.bp.blogspot.com/-oYHqzPtTTlk/Wci8Bvm1e9I/AAAAAAAAfP8/_fyB0vD-9QAoDyzwyTzA3fHOHgEIqebFgCLcBGAs/s72-c/nassari.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/09/nassari-aanika-mazito-madiwani-chadema.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/09/nassari-aanika-mazito-madiwani-chadema.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy