NEYMAR AIONGOZA PSG KUIPIGA MKONO TIMU YA CELTIC

Timu ya Celtic imejuta kuifahamu Paris St-Germain baada ya kupigwa magoli 5-0 katika Mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya huku Neymar akiongoza mauaji.

Mchezaji huyo ghali duniani alifunga kiulani goli la kwanza na kuchangia goli la pili lililofungwa na Kylian Mbappe.

Edinson Cavani akafunga la tatu kwa mkwaju wa penati, Mikael Lustig akajifunga kisha tena Cavani akafunga la tano.
                   Mshambuliaji Kylian Mbappe akifunga goli la pili la Paris St-Germain
Wakati huo huo Barcelona imeibuka na ushindi nyumbani wa magoli 3-0 dhidi ya Juventus huku Lionel Messi akifunga magoli mawili na Ivan Rakitic akifunga moja kwa shuti la mbali.

Lionel Messi akimfunga kipa Gianluigi Buffon hili likiwa ni goli lake la kwanza kuwahi kumfunga kipa huyo
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post