OFISI YA WAKILI WA MANJI YAVAMIWI USIKU

Ofisi ya Mawakili ya Prime Atorneys iliyopo katika jingo la Prime house, Mtaa wa Tambaza, Upanga jijini Dar es Salaam imevamiwa usiku wa manane na watu wasiojulikana na kuchukua kasiki lenye nyaraka mbalimbali pamoja na fedha.
Hudson Nduyepo, mmoja wa mawakili katika ofisi hiyo na miongoni mwa mawakili wanaomtetea mfanyabiashara maarufu Yusuf Manji katika kesi ya uhujumu uchumi, amesema kuwa ofisi yao imevunjwa na wahalifu hao waliomfunga kwa kamba mlinzi na ameenda polisi kutoa taarifa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema limetokea kati ya majira ya saa nane na saa tisa usiku wa kuamkia leo Jumanne Septemba 12.
“Kwa sasa siwezi kusema wahalifu hawa walilenga ofisi gani maana zipo nyingi katika jingo lile. Naomba mtupe nafasi tufanye uchunguzi kisha tutawapa taarifa,” alisema Kamanda Hamduni.
Jengo la Prime House lililopo jirani na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa lina ofisi za kampuni mbalimbali zikiwezo za mawakili, na ofisi za Prime Attorneys zipo katika ghorofa ya tano.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post