PICHA: NYUMBA ZA BILIONEA WA DAR ZITAKAZOPIGWA MNADA LEO NA TRA

Leo Septemba 9, Kampuni ya Udalali ya Yono (Yono Auction Mart) inatarajia kipiga mnada majengo ya ghorofa yanayomilikiwa na Kampuni ya Lugumi Enterprises Limited baada ya mmiliki wake kushindwa kulipa kodi anayodaiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Agosti 20 mwaka huu, kampuni hiyo ilitoa taarifa za kupiga mnada majengo hayo ambayo yapo Upanga na Kigamboni jijini Dar es Salaam baada ya Lugumi kushindwa kulipa deni la kodi analodaiwa na TRA.
Katika tangazo hilo, Yono walieleza kuwa majengo hayo yanaweza kutumiwa kwa ajili ya makazi au ofisi au vyote kwa pamoja.
Scholastica Christian Kevela ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Yono alisema kuwa miezi minne iliyopita nyuma walifungia mali za Lugumi wakimtaka alipe malimbikizo ya kodi aliyokuwa akidaiwa, lakini hadi sasa hajafanya hivyo.
Jana alisema kuwa wametumia njia mbalimbali kuhakikisha kuwa mnada huo unakuwa wa manufaa ambapo walitumia sana vyombo vya habari kufukisha ujumbe kwa umma na kuwaalika kushiriki mnada huo.
Kevela alikataa kutaja kiwango cha fedha ambacho Lugumi anadaiwa na TRA akabaki akisisitiza kwamba ni mabilioni ya shilingi na kwamba TRA ndio wanajua kiwango halisi. Hata hivyo hakutangaza thamani ya majengo hayo akisema kwamba, kila mtanzania aje na fedha aliyonayo kwani wao kama madalali hawana kiwango maalum.
Image result for Nyumba za LugumiImage result for Nyumba za Lugumi

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post