Polisi yazuia mikutano ya Lema

SHARE:

Arusha. Polisi Wilaya ya Arusha imepiga marufuku mikutano ya hadhara ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kwa maelezo kuwa kutakuwa n...Arusha. Polisi Wilaya ya Arusha imepiga marufuku mikutano ya hadhara ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kwa maelezo kuwa kutakuwa na ujio wa viongozi wa kitaifa jijini hapa.
Pia, kuzuiwa mikutano ya mbunge huyo wa Chadema kunahusishwa na tukio la kuungua moto nyumba za polisi.
Katika barua ya Mkuu wa Polisi Wilaya ya Arusha, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP E.Tille kwenda wa Lema jana Jumatano, imeeleza mikutano yake imesitishwa.
Mikutano hiyo ilikuwa ifanyike leo Alhamisi na kesho.
Katika barua hiyo, Jeshi la Polisi limeeleza kuwa tarehe ambazo mikutano hiyo, imepangwa zina mwingiliano na ratiba za shughuli za kiserikali za viongozi wa juu wa Serikali inayoishia Oktoba 4.
Pia, amesema janga la moto katika kambi ya polisi lililotokea jana usiku limeleta madhara makubwa hivyo, nguvu kubwa itaelekewa huko.
"Unashauriwa kupanga mikutano yako tarehe yoyote kuanzia Oktoba 5, 2017  pia rejea mazungumzo yangu na wewe ofisini kwangu ya tarehe 29/09/2017," inasomeka barua hiyo.
Hata hivyo, Lema akizungumza na Mwananchi amesema anapinga polisi kuzuia mikutano yake, kwa kuwa ni ukiukwaji wa sheria na haki za mbunge.
Lema amesema sheria ya Bunge kifungu cha nne fasili ya kwanza, kinazungumzia uhuru        wa mbunge kufanya mikutano jimboni kwake na kifungu cha 4(1) na (2) vinaelezea uhuru huo wa mbunge kufanya mikutano na pia ni ukiukwaji wa sheria kuzuia mikutano ya mbunge kwenye jimbo lake.
Mbunge huyo amesema anaamini, kuzuiwa mikutano yake ni njama kwa kuwa aawali alipanga kuzungumza na wananchi wa Kata ya Kimandolu ambako diwani wao amejiuzulu na wananchi wa Mjini Kati.
"Kwanza waliniita wakaniambia hali ya kisiasa si nzuri nisiende kufanya mkutano Kimandolu kwa kuwa wananchi wanaweza kuwa na hasira baada ya diwani kujiuzulu, mimi nikawaambia wasiwe na hofu lazima likafanye mkutano," amesema.
Lema amesema anajua polisi wanaamini atazungumzia sakata la kupigwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na pia ziara ya Rais John Magufuli ambayo aliifanya hivi karibuni jijini Arusha.
Amesema anashauriana na wanasheria wake kuona kama akubali barua ya polisi au aendelee na mikutano yake.
Hii ni mara ya pili Lema kuzuiwa kufanya mikutano. Agosti 25 alizuiwa ili kupisha mbio za Mwenge wa Uhuru na mitihani ya darasa la saba na alitii agizo hilo.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: Polisi yazuia mikutano ya Lema
Polisi yazuia mikutano ya Lema
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/09/polisi-yazuia-mikutano-ya-lema.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/09/polisi-yazuia-mikutano-ya-lema.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy