RAIS MAGUFULI AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA LA CHAKULA DUNIANI

SHARE:

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula Duniani ( FAO ) Bw. Jose Graziano da Silva amemhakikishia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania M...

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula Duniani (FAO) Bw. Jose Graziano da Silva amemhakikishia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Shirika hilo lipo tayari kushirikiana na Tanzania kufanya mageuzi katika kilimo kwa kuwezesha uzalishaji wa mazao na viwanda vya mazao hayo.
Bw. Jose Graziano da Silva amesema hayo leo tarehe 06 Septemba, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kufanya mazungumzo na Mhe. Rais Magufuli na kumshukuru kwa ushirikiano mzuri ambao shirika hilo limeupata kwa kipindi cha miaka 40 ya uwepo wake hapa nchini.
Akitoa mfano wa nchi yake ya Brazil Bw. Jose Graziano da Silva amesema Tanzania inaweza kupata manufaa makubwa ya kuongeza uzalishaji wa chakula, kuuza nje ya nchi, kuzalisha ajira na kukuza pato la Taifa kupitia mapinduzi yatakayotokana na kuunganisha kilimo na viwanda vikiwemo vya kusindika nyama na samaki kwa kuwa fursa zipo nyingi.
Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli amemshukuru Bw. Jose Graziano da Silva kwa kuja nchini na amemhakikishia kuwa Serikali itaendeleza na kuimarisha zaidi ushirikiano wake FAO, huku akitilia mkazo dhamira yake ya kutaka ushirikiano huo uelekezwe katika ujenzi wa viwanda vya kuzalisha bidhaa zitokanazo na mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi.
“Tanzania ina maziwa mengi, ina ukanda wa bahari wenye urefu wa kilometa 1,422 na ina mito mingi ambayo inaweza kuwekezwa viwanda vya samaki, inashika nafasi ya pili kwa mifugo Barani Afrika, hivyo tunahitaji kujenga viwanda vya nyama.
“Asilimia 75 ya nguvu kazi ya Taifa ni vijana ambao wanauwezo wa kuzalisha mazao mengi ya kilimo tunahitaji viwanda, uchumi wetu ni mzuri na unakua kwa wastani wa asilimi 7.1 na mengine mengi, kwa haya yote tunahitaji wadau ikiwemo FAO tushirikiane kutumia fursa hizi” amesema Mhe. Rais Magufuli na kuahidi kuwa Serikali yake imejipanga kusimamia miradi yoyote itakayoletwa nchini ili itekelezwe kwa uadilifu na ubora wa hali ya juu.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amefanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Mzee Joseph Butiku Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Baada ya mazungumzo hayo Mzee Butiku amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya kuongoza Serikali ambapo katika kipindi kifupi amesimamia vizuri nidhamu, watu kufanya kazi, kupiga vita rushwa, ulipaji wa kodi na amemtaka asirudi nyuma kwa kuwa nchi inakwenda vizuri.
“Mimi nimefanya kazi hapa Ikulu kwa miaka 23, Mwl. Nyerere alijenga misingi mizuri, lakini huyu Rais Magufuli ameisimamia vizuri sana, unapofanya mambo kama haya, lazima hapa nyumbani na huko nje kutakuwa na maneno, mazuri sikiliza, ya hovyo achana nayo” amesisitiza Mzee Butiku.
Katika hatua nyingine, Mhe. Rais Magufuli ameagana na Balozi wa China hapa nchini anayemaliza muda wake Mhe. Dkt. Lu Youqing na kumshukuru kwa kazi kubwa na nzuri aliyoifanya katika kipindi cha miaka mitano aliyokuwepo hapa nchini.
Mhe. Rais Magufuli amesema katika kipindi chake Mhe. Dkt. Lu Youqing ametoa mchango mkubwa katika kuendeleza na kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano kati China na Tanzania, uliofanikisha kuongeza uwekezaji katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu, elimu, kilimo, afya na kukuza biashara ambapo wafanyabiashara wengi wa China wamekuja kuwekeza nchini, mambo ambayo yamezalisha ajira na kukuza pato la nchi.
Mhe. Dkt. Magufuli amemuomba Mhe. Dkt. Lu Youqing kuendelea kuitangaza vyema Tanzania nchini China, ambako anakwenda kushughulikia masuala ya uchumi na kwamba anaamini atatumia nafasi hiyo kuhimiza wawekezaji na wafanyabiashara wengi zaidi wa China kuja kuwekeza hapa nchini.
“Mhe. Balozi Dkt. Lu Youqing Watanzania hatutakusahau kwa mchango wako, wewe ni ndugu na rafiki yetu, tunakushukuru sana kwa yote uliyoifanyia nchi yetu, naomba nikuhakikishie kuwa kazi nzuri uliyoifanya tutaiendeleza na tutashirikiana na Balozi mpya atakayekuja kuendeleza pale ulipoachia” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Kwa upande wake Mhe. Dkt. Lu Youqing amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa ushirikiano alioupata kwa kipindi chote alichokuwepo hapa nchini na ameahidi kuwa ataendelea kuwa Balozi mzuri wa kuinadi Tanzania huko nchini China.
“Mhe. Rais Magufuli nakushukuru sana, hapa Tanzania ni nyumbani kwangu na nipo tayari wakati wote kutoa ushirikiano pale nitakapohitajika kufanya hivyo kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini China ama kutoka Serikalini hapa Tanzania” Amesema Dkt. Lu Youqing.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
06 Septemba, 2017

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: RAIS MAGUFULI AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA LA CHAKULA DUNIANI
RAIS MAGUFULI AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA LA CHAKULA DUNIANI
https://4.bp.blogspot.com/-T5ajXWwVPmk/WbAVqZGk16I/AAAAAAAAeYE/SMuHDqAcDuY1FGaWnbnxq0PKAjrUmYg_QCLcBGAs/s1600/xIMG_8103-1-2-750x375.jpg.pagespeed.ic.SW8A2_N4L8.webp
https://4.bp.blogspot.com/-T5ajXWwVPmk/WbAVqZGk16I/AAAAAAAAeYE/SMuHDqAcDuY1FGaWnbnxq0PKAjrUmYg_QCLcBGAs/s72-c/xIMG_8103-1-2-750x375.jpg.pagespeed.ic.SW8A2_N4L8.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/09/rais-magufuli-akutana-na-mkurugenzi.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/09/rais-magufuli-akutana-na-mkurugenzi.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy