RATIBA: MECHI ZA VPL WIKIENDI HII

Mzunguko wa Tatu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), inatarajiwa kuendelea mwishoni mwa wiki hii. 


Kwa mujibu wa ratiba ya VPL, kesho Ijumaa Septemba 15, 2017 Azam FC itaialika Kagera Sugar saa 1.00 usiku (19h00) katika Uwanja wa Azam ulioko Chamazi jijini Dar es salaam.
Kwa siku ya Jumamosi Septemba 16, 2017 Majimaji FC ya Songea itacheza na Young Africans ya Dar es Salaam, saa 10.00 jioni (16h00) katika Uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma.
Mbao itasafiri hadi Manungu mkoani Morogoro kucheza na Mtibwa Sugar katika mchezo ambao pia utapigwa Jumamosi saa 16h00 wakati Tanzania Prisons ya Mbeya itakuwa mwenyeji wa Ndanda FC saa 16h00 kwenye Uwanja wa Sokoine.
Lipuli Fc itakuwa mwenyeji wa Ruvu Shooting saa 16h00 katika Uwanja wa Samora, Iringa wakati Stand United itacheza na Singida United saa 16h00 kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
Siku ya Jumapili Septemba 17, 2017 Mbeya City itaikaribisha Njombe Mji saa 16h00 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya huku Simba SC ikiwa mwenyeji wa Mwadui FC saa 16h00 jioni katika Uwanja wa Uhuru, Dar es salaam.

OKWI MCHEZAJI BORA MWEZI AGOSTI 2017
 
Mshambuliaji wa Simba ya Dar es Salaam, Emmanuel Okwi amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Agosti wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2017/2018.

Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini

http://tff.or.tz/news/694-okwi-mchezaji-bora-mwezi-agosti-2017
 
TFF YATOA UTARATIBU WA MAWASILIANO
 
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), lingependa kutoa maelekezo ya kufuatwa kwa utaratibu wa mawasiliano kwa mfumo wa halakia yaani ngazi moja baada ya nyingine kwa ukubwa.

Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini

http://tff.or.tz/news/693-tff-yatoa-utaratibu-wa-mawasiliano
 
KARIBU LIGI DARAJA LA KWANZA MSIMU WA 2017/18
 
Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inatarajiwa kuanza Jumamosi Septemba 16, 2017 katika viwanja vinne tofauti nchini kwa mujbu wa ratiba iliyotoka mwezi uliopita.

Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini

http://tff.or.tz/news/692-karibu-ligi-daraja-la-kwanza-msimu-wa-2017-18
 
UPUNGUFU LESENI ZA KLABU
 
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetoa muda kwamba hadi Septemba 22, klabu zote 16 za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) na za zile 24 Ligi Daraja la Kwanza (FDL), ziwe zimekamilisha taratibu za kupata Leseni za Klabu.

Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini

http://tff.or.tz/news/691-upungufu-leseni-za-klabu
 
THE TANZANITE YAENDA NIGERIA
Timu ya Taifa ya Tanzania ya wanasichana wenye umri wa chini ya miaka 20 ‘The Tanzanite’ imeondoka usiku wa kuamkia leo Alhamisi kwenda Nigeria kwa Ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia.
 
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini

http://tff.or.tz/news/690-the-tanzanite-yaenda-nigeria
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post