RIPOTI YA UFISADI WA MADINI YA TANZANITE NA ALMASI MIKONONI MWA RAIS MAGUFULI

tarehe 07 Septemba, 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli atapokea taarifa ya uchunguzi wa madini ya Tanzanite na Almasi uliofanywa na kamati maalum mbili zilizoundwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai.
Taarifa hiyo itakabidhiwa kwa Rais Magufuli na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Hafla ya kukabidhiwa kwa taarifa hiyo itarushwa moja kwa moja na vituo vya redio na televisheni kuanzia saa 4:00 Asubuhi.
Wananchi wote mnaombwa kufuatilia matangazo hayo kupitia vyombo vya habari na tovuti rasmi ya Ikulu ambayo ni www.ikulu.go.tz
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
06 Septemba, 2017
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

SHARE THIS

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post