RISASI ZA TUNDU LISSU ZAMPONZA MBUNGE WA UBUNGO

Spika wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai leo Jumanne, Septemba 12, ameagiza kutafutwa kwa Mbunge wa Jimbo la Ubungo (CHADEMA), Saed Kubenea na kupelekwa katika Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama.
Spika Ndugai amesema anatakiwa kuhojiwa kuhusu kauli aliyoitoa akimtuhumu Spika kuwa amedanganya idadi ya risasi alizopigwa Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu.
Vile vile Spika ameagiza Mbunge huyo kufikishwa katika Kamati ya Bunge ya Maadili na Madaraka pamoja na Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT Wazalendo), Zito Kabwe kwa tuhuma mbili tofauti.
Zitto Kabwe anatuhumiwa kutamka kuwa Bunge limewekwa mfukoni na muhimili fulani, huku Kubenea akifikishwa kwa kumtuhumu Spika kudanganya idadi ya risasi alizopigwa Lissu.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post