Serikali haijui Ben Saanane kama amekufa au yuko hai

SHARE:

Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amesema Serikali haijui kama Ben Saanane alikufa au yuko hai, lakini Je...
Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amesema Serikali haijui kama Ben Saanane alikufa au yuko hai, lakini Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta ili kujua kilichotokea.
Saanane ambaye ni Mkuu wa Idara ya Sera na Utafiti wa Chadema na Msaidizi wa mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe alitoweka tangu Novemba 2016.
Amesema hayo leo Alhamisi katika kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na kituo cha televisheni cha Clouds alipojibu swali aliloulizwa na mtangazaji wa kipindi hicho iwapo Ben Saanane yuko hai au amefariki dunia.
“Ni ngumu kusema kama Ben Saanane yuko hai au amefariki kwa sababu bado hatujui nini kilimpata,” amesema.
Amesema Polisi wanaendelea kumtafuta kwa kuwa ni mtu aliyepotea. Amewataka watu wenye taarifa zinazoweza kusaidia kupatikana kwake watoe ushirikiano.
“Msidhani kwamba Serikali haifanyi chochote, suala ambalo linahusisha maisha ya mtu hatulipuuzi tunaendelea na upelelezi,” amesema.
Kuhusu mtu aliyemtishia bastola aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amesema wamejiridhisha kwamba hakuwa polisi.
“Kwanza tulitaka kufahamu yule jamaa aliyefanya kitendo kile kama alikuwa polisi lakini tulikuja kufahamu kwamba hakuwa polisi,” amesema.
Amesema katika mazingira kama yaliyotokea yanaweza kutumiwa na mhalifu yeyote kufanya alichokifanya. Amesema bado wanalifanyia uchunguzi suala hilo.
Hata hivyo, Mwigulu hakujibu swali aliloulizwa iwapo mtu huyo amekamatwa au hajakamatwa hadi sasa.
Machi 23, Nape alitishiwa kwa bastola wakati alipofika katika Hoteli ya Protea kwa ajili ya kuzungumza na waandishi wa habari.
Tukio hilo lilitokea saa chache baada ya  Rais John Magufuli kufanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri yaliyomwondoa Nape kwenye nafasi ya uwaziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,73,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,273,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,13,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,567,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3301,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,333,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,386,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,68,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1379,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1286,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: Serikali haijui Ben Saanane kama amekufa au yuko hai
Serikali haijui Ben Saanane kama amekufa au yuko hai
http://zotekaliblog.com/wp-content/uploads/2017/09/picsaanane.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/09/serikali-haijui-ben-saanane-kama.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/09/serikali-haijui-ben-saanane-kama.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy