SERIKALI KUENDELEA KUIWEZESHA MUHIMBILI KUTOA HUDMA ZA KIBINGWA

SHARE:

Na John Stephen, Muhimbili  Dar es Salaam, Tanzania. Serikali imesema itaendelea kuiwezesha Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) katika mika...

Na John Stephen, Muhimbili 

Dar es Salaam, Tanzania. Serikali imesema itaendelea kuiwezesha Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) katika mikakati yake ya kutoa huduma bora za afya zikiwamo za ubingwa wa hali ya juu pamoja na upasuaji katika maeneo mbalimbali. 

Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu katika hospitali hiyo wakati akizindua vyumba viwili vya upasuaji wa watoto wadogo (Pediatrick operating theatres) vyenye thamani ya Dola za Marekani 675,000 sawa na Tsh. 1.5 bilioni pamoja na uzinduzi wa wodi ya watoto yenye vitanda 25. 

Katika uzinduzi huo Waziri Mwalimu ameitaka Muhimbili kutokutoa rufaa kwa mgonjwa yoyote ambaye anaweza kupatiwa mabatibabu katika hospitali hiyo. 

“Narudia tena, hata kama ni mimi au kiongozi yoyote asipewe rufaa kama ugonjwa wake unaweza kutibiwa hapa, mimi naweza kuja hapa nikawashinikiza mnipeleke nje, msikubali, simamieni taaluma yenu. Kama madaktari wamezibitisha mgonjwa anaweza kutibiwa hapa, hakuna haja ya kupelekwa nje,” Mhe. Ummy. 

Vyumba hivyo vya upasuaji vimewekewa vifaa vya upasuaji kwa msaada wa mfuko wa ARCHIE WOOD FOUNDATION ya Scotland. 


“Napenda kuwashukuru kwa namna ya pekee wahisani wetu Sir.Ian Wood na mtoto wako Garret Wood ambao mlipoletewa wazo la kuisaidia Hospitali ya Taifa Muhimbili kupitia taasisi yenu ya Archie Wood Foundation mlilipokea kwa mikono miwili na kulitekeleza. 

Nichukue nafasi hii kwa niaba ya Serikali chini ya Uongozi wa wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwashukuru sana kwa msaada huu,” amesema Waziri Ummy Mwalimu. 

Waziri ameutaka uongozi wa Muhimbili kuweka mpango mzuri wa matengenezo kinga ili kuhakikisha kila kifaa kinatunzwa na kutumika kwa lengo lililokusudiwa. 

Naye Mkurugenzi wa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru amefafanua kuwa msaada uliotolewa na mfuko huo kuwa ni taa za kufanyia upasuaji (operating lights), mashine za usingizi (anesthetic machines with monitors), mashine za kuzuia damu isiendelee kupotea wakati wa upasuaji (diathermy machines), mashine ya kutasisha vifaa vya upasuaji na vifaa vyake, vitanda vya kufanyia upasuaji (operating tables) na vifaa mbalimbali vya upasuaji (surgical kits). 

Profesa Museru amesema kuwa leo wamepatiwa vifaa vya kisasa kwa kutumia vyumba hivyo viwili na kwamba upasuaji utakuwa ikifanyika mara 10 kwa wiki badala ya mara tatu kwa wiki kama ilivyokuwa awali. 

“Hii itaondoa kero ya msongamano kwa watoto wanaohitaji kufanyiwa upasuaji wakati mwingine ilibidi wasubiri kwa muda wa miaka miwili ili kufanyiwa upasuaji,”amesema Profesa Museru.
001

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (katikati) akizindua vyumba viwili vya upasuaji wa watoto wadogo leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Wood na Archie, Sir. Ian Wood na maofisa wengine wakiwa kwenye uzinduzi huo leo.

002
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akiangalia baadhi ya vifaa vilivyotolewa na Mfuko wa Wood na Archie katika vyumba vya upasuaji wa watoto wadogo kwenye hospitali hiyo.
003
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza kabla ya kuzindua vyumba vya upasuaji wa watoto. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru, Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa Muhimbili, Dk. Julieth Magandi na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wood na Archie, Ian Wood akiwa kwenye mkutano huo leo.
004
Baadhi ya watoto wanaotibiwa katika hospitali hiyo wakiwamo madaktari, wauguzi na baadhi ya watumishi wakimsikiliza Waziri Ummy Mwalimu leo.
005
Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru akizungumza leo kwenye mkutano huo kabla ya kuzinduliwa kwa vyumba vya upasuaji wa watoto.
006
Baadhi ya watumishi wa Muhimbili wakifuatilia mkutano huo leo
007
Profesa George Youngson akizungumza kwenye mkutano huo leo kabla ya kukabidhi vyumba vya upasuaji na wodi ya watoto yenye vitanda 25. Pembeni ni timu ya wataalamu wa Wood na Archie Foundation.
008
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Wood na Archie, Sir. Ian Wood akizungumza katika mkutano huo leo.
009
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Wateja, Aminiel Aligaesha akiwa na mmoja wa watoto ambaye amemweleza Waziri Ummy Mwalimu kwamba ndoto yake ni kuwa daktari. Waziri ameahidi kumsomesha mtoto ili kufikia ndoto yake. 

PICHA NA JOHN STEPHEN, HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: SERIKALI KUENDELEA KUIWEZESHA MUHIMBILI KUTOA HUDMA ZA KIBINGWA
SERIKALI KUENDELEA KUIWEZESHA MUHIMBILI KUTOA HUDMA ZA KIBINGWA
https://3.bp.blogspot.com/-S4cL-eZj65s/WckX1iAq_mI/AAAAAAAAfQg/WOUDcwcgM4wjMxR6qtNGhSWmtVAD7451wCLcBGAs/s1600/xMNH-Welcome-SIgn-640x375.jpg.pagespeed.ic.UDGxt1WBCs.jpg
https://3.bp.blogspot.com/-S4cL-eZj65s/WckX1iAq_mI/AAAAAAAAfQg/WOUDcwcgM4wjMxR6qtNGhSWmtVAD7451wCLcBGAs/s72-c/xMNH-Welcome-SIgn-640x375.jpg.pagespeed.ic.UDGxt1WBCs.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/09/serikali-kuendelea-kuiwezesha-muhimbili_25.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/09/serikali-kuendelea-kuiwezesha-muhimbili_25.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy