SERIKALI YACHUKUA SHAMBA JINGINE YA MANJI AKIWA RUMANDE

Serikali imefuta umiliki wa shamba la mfanyabiashara Yusuf Manji, lenye ukubwa wa ekari 71 lililokuwa Wilayani Kigambo Dar es Salaam baada ya mmiliki huyo wa awali kushindwa kuliendeleza.
Hayo yamewekwa wazi na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi na kusisitiza kwamba asione mtu yoyote anavamia mashamba hayo yaliyofutiwa umiliki hadi hapo yatakapopangiwa matumizi mengine.
Mbali na shamba la Manji, shamba jingine la kampuni ya Amadori lenye ukubwa wa ekari 5,400 nalo limefutiwa umiliki ikiwa ni muondelezo wa serikali kuyatwaa mashamba makubwa ambayo hayajaendelezwa.
Waziri alisema kuwa, ufutaji huu ni baada ya wamiliki hao kushindwa kuyaendeleza na kuwanyima fursa wananchi kufanya shughili zingine na kuinyima wilaya kufanya shuguli za viwanda na uwekezaji mwingine kutokana na kuhodhi kwa maeneo hayo.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post