SERIKALI YAELEZA ADHABU KWA WATUMISHI WATAKAOVUJISHA SIRI

SHARE:

Na. Georgina Misama – MAELEZO Serikali kupitia Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imewaonya watumishi wa Um...

Na. Georgina Misama – MAELEZO
Serikali kupitia Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imewaonya watumishi wa Umma kutoa taarifa za serikali za siri na za kawaida kwa watu ambao sio walengwa wa taarifa hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Maadili kutoka Wizara hiyo Lambert Chialo alisema kwamba kwa mujibu wa Sheria ya Usalama wa Taifa Na. 3 ya mwaka 1970 na marekebisho yake, Ibara ya 5(a) na (b), adhabu ya uvujaji wa siri ni kifungo kisichozidi miaka 20.
“Hivi karibuni tumeshuhudia taarifa za serikali za siri zikitumwa katika vyombo vya habari pamoja na mitandao mbalimbali ya kijamii kitu ambacho ni kosa kisheria na ni kinyume cha Kanuni za Maadili ambapo inasisitizwa kuwa na matumizi sahihi ya taarifa”, alisema Chialo.
Chialo aliongeza kwamba lengo la serikali si kuficha taarifa kwa wadau wake, bali taarifa zinazotolewa zinapaswa kutolewa kwa utaratibu maalumu na kupelekwa kwa watu wanaopaswa kupokea taarifa hizo (walengwa). Aidha, taarifa zinazotolewa na taasisi husika lazima zipate idhini kwa Uongozi husika kabla ya kupelekwa kwa wadau.
Akiongelea suala la matumizi mabaya ya Ofisi, Chialo alisema kwamba baadhi ya watumishi wamekuwa wakitumia nafasi walizonazo kwa  manufaa yao binafsi na sio ya Umma, kwa kufanya hivyo ni kosa kisheria na watumishi watakaogundulika watawajibishwa kwa mujibu wa Kanuni na taratibu.
Watumishi wa Umma wanapaswa kufahamu kwamba serikali inaendelea kufatilia matendo yote yasiyo ya kimaadili na kuchukua hatua kila inapobidi. Aidha, wananchi wanaombwa kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za ukiukwaji wa maadili katika taasisi za umma kila wanaposhuhudia matukio hayo.
“Tunalo dawati la msaada kwa ajili ya kupokea maoni, malalamiko, ushauri na taarifa mbalimbali katika kuhakikisha utoaji wa huduma za serikali kwa wananchi unaboreshwa” alisema Chialo.
Chialo alitoa rai kwa wananchi wote kwa ujumla, kuzingatia swala la maadili kuanzia ngazi ya familia. Aidha, inasisitizwa viongozi na wasimamizi wa kazi kuendelea kuelimisha watumishi kuhusu suala la maadili na kuhakikisha watumishi wanaishi kwa kuzingatia kanuni na taratibu zilizopo kwa vitendo.
MWISHO.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: SERIKALI YAELEZA ADHABU KWA WATUMISHI WATAKAOVUJISHA SIRI
SERIKALI YAELEZA ADHABU KWA WATUMISHI WATAKAOVUJISHA SIRI
https://4.bp.blogspot.com/-uqsgxzpHYp4/Wbg7DG0216I/AAAAAAAAeos/AJbpaDEPDQwow7TqIhTtS-Wjw2p20hmwACLcBGAs/s1600/xPix-01-1-750x375.jpg.pagespeed.ic.5Trd5qcG2S.webp
https://4.bp.blogspot.com/-uqsgxzpHYp4/Wbg7DG0216I/AAAAAAAAeos/AJbpaDEPDQwow7TqIhTtS-Wjw2p20hmwACLcBGAs/s72-c/xPix-01-1-750x375.jpg.pagespeed.ic.5Trd5qcG2S.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/09/serikali-yaeleza-adhabu-kwa-watumishi.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/09/serikali-yaeleza-adhabu-kwa-watumishi.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy