SERIKALI YASEMA ITAMKUMBUKA SISTA JEAN PRUITT KWA MAMBO MENGI

SHARE:

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura amesema kwamba Mwanzilishi wa Nyumba ya Sanaa pamoja na Vituo ...

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura amesema kwamba Mwanzilishi wa Nyumba ya Sanaa pamoja na Vituo mbalimbali vya Sanaa na Utamaduni nchini Tanzania, marehemu Sista Jean Pruitt atakumbukwa kwa utu, upendo na kujituma wakati wote na kujitoa kwake kwa hali na mali katika kuviendeleza Vituo mbalimbali vya Sanaa na Utamaduni pamoja na kuendeleza maisha ya wenye mahitaji.
Wambura ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya Karimjee wakati wa Ibada ya kumuaga mtawa huyo aliyefariki dunia siku za hivi karibuni Jijini Arusha.
Amesema kwamba, mtawa huyo amekuwa akifanya kazi zake kwa bidii kwa kipindi cha zaidi ya miaka 40 kwa ajili ya kuwasaidia Watanzania na baadhi ya vituo ambavyo alivianzisha ni pamoja na Kituo cha Dogodogo Centre, TAMOFA, Vipaji, Alliance, huku akisaidia maendeleo ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) katika kukuza vipaji vya vijana mbalimbali nchini.
“Sista Jean atakumbukwa kwa jinsi alivyojitoa kusaidia na kuleta mabadiliko katika tasnia ya sanaa ikiwemo kutumia Nyumba ya Sanaa katika kuibua na kuviendeleza vipaji vya sanaa kwa Vijana wetu nchini,” alisema Mhe. Wambura.
Aliongeza kuwa, mchango wake katika sanaa ulimwezesha mtawa huyo kupata tuzo mbalimbali zikiwemo, mwaka 1983 alipewa Tuzo Maalum na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambayo ilikua Tuzo ya Maisha pamoja na Tuzo ya Zeze iliyotolewa na uliokuwa Mfuko wa Utamaduni Tanzania.
Akisoma wasifu wa mtawa huyo, Mwakilishi wa Shirika la Masista wa Maryknoll, amesema kwamba, Sista Jean Pruitt alikuja Tanzania 1968 akifanya mambo mbalimbali kwa jamii ikiwemo masuala ya sanaa na watoto wadogo hususani wale wanaotoka katika mazingira magumu hivyo kazi zake alitekeleza kwa vitendo kuliko maneno.
“Sista Jean Pruitt alifanya shughuli mbalimbali ikiwemo miradi kwa vitendo zaidi, pia aliwalea watoto wengi zaidi nchini Tanzania kwa kuwasomesha na kuwasaidia vijana kuibua vipaji vyao,” alisema Mwakilishi huyo.
Marehemu sista Jean Pruitt alizaliwa nchini Marekani Oktoba 17, 1939 katika Jimbo la Michigan na alijihusisha sana na masuala ya ustawi wa jamii akijikita katika masuala ya Sanaa na Watoto hususani nchini Tanzania pia ndiye mwanzilishi wa Nyumba ya Sanaa.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: SERIKALI YASEMA ITAMKUMBUKA SISTA JEAN PRUITT KWA MAMBO MENGI
SERIKALI YASEMA ITAMKUMBUKA SISTA JEAN PRUITT KWA MAMBO MENGI
https://4.bp.blogspot.com/-ftkC-RqcOtk/WcKZ-xLSE0I/AAAAAAAAfAY/fnenQZCHG3IruscGBCpn-U79yhRB4T2DQCLcBGAs/s1600/PICHA-4-2-750x375.jpg
https://4.bp.blogspot.com/-ftkC-RqcOtk/WcKZ-xLSE0I/AAAAAAAAfAY/fnenQZCHG3IruscGBCpn-U79yhRB4T2DQCLcBGAs/s72-c/PICHA-4-2-750x375.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/09/serikali-yasema-itamkumbuka-sista-jean.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/09/serikali-yasema-itamkumbuka-sista-jean.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy