SERIKALI YAUCHUKUA UWANJA WA NDEGE ULIOKUWA UNAMILIKIWA NA ACACIA

Siku chache baada ya Kampuni ya uchimbaji wa madini ya Acacia kutangaza kusudio la kupunguza utendaji kazi katika Mgodi wa Bulyanhulu, kampuni hiyo imekabidhi Serikalini baadhi ya mali zake kwenye Mgodi wa Buzwagi ambao unatarajiwa kufungwa miaka mitatu ijayo.
Jana Septemba 5, 2017 kampuni hiyo iliikabidhi Serikali uwanja wa ndege uliopo katika mgodi huo. Mgodi huo ni wa pili kufungwa na kampuni hiyo baada ya ule wa Tulawaka ambao iliuuza kwa Shirika la Taifa la Madini (STAMICO) mwaka 2013.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack alisema hiyo ni hatua ya awali katika mchakato wa mgodi huo kusitisha shughuli zake za uchimbaji madini kwa mujibu wa mkataba uliopo.
“Tumeanza na uwanja wa ndege baadae tutakabidhiwa majengo na vitu vingine kama ulivyo utaratibu,” alisema Telack.
Alisema Disemba mwaka huu utakuwa mwisho wa shughuli za uchimbaji na baada ya hapo wataanza kusaga mawe yaliyochimbwa kwa miaka mitatu mfululizo mpaka 2020.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post