SERIKALI YAWADHIBITI WALANGUZI WA BEI YA MBOLEA

SHARE:

Na. Eliphace Marwa – Maelezo Serikali imeingiza nchini jumla ya tani elfu 32 za mbolea ya kukuzia pamoja na tani elfu 23 za mbolea ya k...

Na. Eliphace Marwa – Maelezo
Serikali imeingiza nchini jumla ya tani elfu 32 za mbolea ya kukuzia pamoja na tani elfu 23 za mbolea ya kupandia kupitia mfumo mpya wa uagizaji wa mbolea kwa pamoja, lengo likiwa ni kudhibiti bei kwa kuzingatia bei elekezi.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam wakati zoezi la upakuaji wa mbolea hiyo likiendelea Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Udhibiti wa Ubora wa Mbolea Tanzania (TFRA) Bw. Lazaro Kitandu amesema kuwa mpaka sasa jumla ya tani elfu 55 za mbolea zimewasili nchini.
Hii ni awamu ya kwanza ya kuingiza mbolea nchini kupitia mfumo mpya ya uagizaji mbolea kwa pamoja ambapo kampuni ya OCP S.A ya nchini Morocco imeingiza jumla ya tani elfu 23 za mbolea ya kupandia na Kampuni ya Premium Agro Chem imeingiza tani elfu 32 za mbolea ya kukuzia.
“Mpaka sasa zoezi la kupakua mbolea ya kupandia (DAP) tani elfu 23 linaendelea vizuri na mara baada ya kumaliza kupakua mbolea hii tutaanza zoezi la kupakua mbolea ya kukuzia (UREA) ambayo ni tani elfu 32,” alisema Bw. Kitandu.
Kitandu aliongeza kuwa Mheshimiwa Waziri wa kilimo juzi alipokuwa anaongea na waandishi wa habari mjini Dodoma na akasisitiza bei ambazo zimetolewa zisimamiwe na kila ngazi kwasababu taasisi peke yake haiwezi kuwa na watu kila mahali hivyo Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa mpaka Kijiji zitasaidia kusimamia bei ambazo zimetolewa.
Pia Kitandu aliongeza kuwa kuhusiana suala la bei ya mbolea hiyo itatangazwa kupitia vyombo vya habari kama vile magazeti na televisheni na hivyo kutoa onyo kwa mawakala kujipangia bei kwa kuuza mbolea nje ya bei elekezi ya Serikali kwamba watachukuliwa hatua za kisheria kama kunyang’anywa leseni, kufungwa, faini au vyote kwa pamoja.
Aidha Kitandu alisisitiza kuwa mbolea hizi siyo mbolea za ruzuku kwani wakulima wengi wamekuwa wakichanganya mbolea hizi na mbolea za ruzuku na amefafanua kuwa mbolea hii imefanyiwa utaratibu wa kudhibiti toka kule inapotoka na hivyo serikali itahakikisha mbolea hii inauzwa kwa kulingana na bei ya soko la dunia.
Aidha Bw. Kitandu  aliwahakikishia wakulima kuwa  mbolea itasafirishwa mpaka vijijini kwa kutumia treni na malori kwa sehemu ambapo treni haiwezi kufika, na amewatoa hofu wakulima kuwa msimu unaoanza mwezi huu wameingiza tani 23,000 kwa mbolea ya kupandia (DAP) na tani 32,000 kwa mbolea ya kukuzia (UREA) ambapo watakuwa wanaagiza kwa awamu kwa miezi miwili miwili.
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari nchini wakiendelea na zoezi la upakiaji wa mbolea ya kupandia tani elfu 23 tayari kwenda kwa wakulima mapema hii leo jijini Dar es Salaam.Wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari nchini wakiendelea na zoezi la kufunga mbolea ya kupandia
katika mifuko tayari kwa kupakiwa na kusafirishwa kwenda kwa wakulima.
Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Udhibiti wa Ubora wa Mbolea Tanzania (TFRA) Bw. Lazaro Kitandu (katikati) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari wakati zoezi la upakuaji wa mbolea ya kupandia ukiendelea katika bandari ya Dar es Salaam mapema hii leo.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,265,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3244,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,329,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,382,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,345,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1356,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1277,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,131,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: SERIKALI YAWADHIBITI WALANGUZI WA BEI YA MBOLEA
SERIKALI YAWADHIBITI WALANGUZI WA BEI YA MBOLEA
https://2.bp.blogspot.com/-Eg4wF_Cl97U/Wba9vsXJFpI/AAAAAAAAekc/zqSzq-eBymEtycLph4EExmGrrWZ8pT-dwCLcBGAs/s1600/DJdDo1BXUAAyxih.jpg
https://2.bp.blogspot.com/-Eg4wF_Cl97U/Wba9vsXJFpI/AAAAAAAAekc/zqSzq-eBymEtycLph4EExmGrrWZ8pT-dwCLcBGAs/s72-c/DJdDo1BXUAAyxih.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/09/serikali-yawadhibiti-walanguzi-wa-bei.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/09/serikali-yawadhibiti-walanguzi-wa-bei.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy