SHILOLE AWEKA WAZI TAREHE YA NDOA YAKE

Mwanamuziki maarufu na muigizaji wa filamu nchini Tanzania Zuwena Mohamed anayejulikana kwa jina la kisanii ‘Shilole’ ambaye alificha kwa muda mrefu mahusiano yake ya kimapenzi kwa madai kuwa haujafika muda muafaka wa kuyasema hadharani, sasa ametaja siku ambayo atafunga ndoa yake.
Shilole ameeleza kuwa atafunga ndoa na mpenzi wake wa sasa Ashrafu Uchebe Desemba 20 mwaka huu ambayo ndiyo siku atakayoadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.
Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya akaunti moja ya instagram yenye jina la Uchebe kusemekana kuandika maneno ya kejeli dhidi ya mwanamuziki Shilole.
Alieleza kuwa akaunti hiyo siyo ya mpenzi wake na waliotengeneza walikuwa na lengo la kumchafulia jina na sifa yake yeye pamoja na mpenzi wake.
“Mpenzi wangu hana akaunti hiyo, watu wanataka kutuharibia. Sasa nawaambia wameshindwa na tunafunga ndoa,” Alisema Shilole.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post