TAMKO LA MAREKANI JUU YA KUSHAMBULIWA KWA TUNDU LISSU

Marekeani imeeleza kuwa imesikitishwa na tukio la kikatili la kushambuliwa kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu akiwa anaelekea nyumbani kwake Dodoma eneo la Area D akitokea bungeni majira ya saa 7 mchana.
Kupitia ukurasa wa Facebook wa Ubalozi wa marekani imechapishwa taarifa inayosema “Tunalaani kitendo hiki cha kipuuzi na cha kutumia nguvu”
Ubalozi huo umesema kuwa unaungana na watanzania wote katika kumtakia kheri Tundu Lissu ilia pone haraka na arejee katika afya yake.
Tundu Lissu ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) jana usiku alisafirishwa kuelekea katika hospitali ya Aga Khan, Jijini Nairobi kwa ajili ya matibabu zaidi baada ya kupatiwa matibabu ya awali katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma.
Spika wa Bunge, Job Ndugai leo asubuhi akiwa bungeni alisema kuwa gari la Lissu lilifyatuliwa risasi 28 hadi 32 na kati ya hizo tano zilimpata katika mwili wake.
Aliendelea kusema kuwa risasi mbili zilimpata lissu kwenye miguu, mbili tuumboni na moja kwenye mkono.
Jeshi la Polisi bado linaendelea na upelelezi wa tukio hilo na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano ili kusaidia kufanikishwa kupatikana kwa wahalifu waliohusika katika shambulio hilo.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post