TMA YATAJA MIKOA ITAKAYOKUMBWA NA UKAME WAKATI VULI

Mamlaka ya Utabiri wa Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa hali ya hewa katika robo ya nne ya mwisho mwaka 2017 (Oktoba – Disemba) ambapo kwa mujibu wa ripoti hiyo inaonyesha kuwa baadhi ya maeneo yanatarajia kuwa na mvua za wasatani hadi juu ya wastani huku nyingine zikitarajia mvua za wastani na chini ya wastani.
Katika taarifa hiyo ya TMA imeonyesha kuwa, kutakuwa na mtawanyiko hafifu wa mvua na vipindi virefu vya ukavu vinavyotarajiwa kujitokeza katika baadhi ya maeneo husasani katika kipindi cha miezi ya Oktoba hadi Novemba, 2017 kwa maeneo ya Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki na Pwani ya Kaskazini.
Dk Agness Kijazi ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa TMA alisema kuwa mvua za wastani na chini ya wastani na vipindi virefu vya ukame vinatarajiwa katika maeneo ya Magharibi mwa Ziwa Victoria, Pwani ya Kaskazini, Mkoa wa Kilimanjaro na Kaskazini
mwa ,Mkoa wa Kigoma.
Aidha, TMA imeeleza kuwa, Mikoa ya Arusha na Manyara pamoja na maeneo ya Mashariki na Kusini mwa Ziwa Victoria yanatarajiwa kuwa na mvua za wastani hadi juu ya wastani.
Mvua za Vuli, 2017 zinatarajiwa kuanza mwezi Septemba, 2017 katika maeneo mengi ya Ziwa Viktoria na mwezi Oktoba, 2017 katika ukanda wa pwani, na baadaye mwezi Novemba katika maeneo ya nyanda za juu kaskazini mashariki. Ongezeko la mvua linatarajiwa katika miezi ya Novemba na Disemba, 2017 na hali kadhalika vipindi virefu vya ukavu vinatarajiwa kujitokeza zaidi katika mwezi wa Oktoba, 2017.
TMA imetoa ushauri kuwa, wakulima waandae mashamba yao mapema na kupanda mazao yanayokomaa katika muda mfupi kwa kufuata ushauri wa wataalam wa kilimo. Wafugaji wameshauriwa kuvuna mifugo yao ikiwa katika hali nzuri kiafya na pia kuvuna maji na kuhifadhi malisho ili kukidhi mahitaji katika kipindi cha upungufu.
TMA imezitaka mamlaka nyingine zikiwemo za maafa na vyombo vya habari kuchukua tahadhari ili kuepuka madhara yanayoweza kutokana kutokana na uwepo wa vipindi vya ukame.
Hapa chini ni taarifa rasmi ya TMA kuhusu hali ya hewa iliyotole Septemba 4, 2017.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post