TUNDU LISSU HATIBIWI HOSPITALI YA AGA KHAN NAIROBI

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeeleza kuwa Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki, Tundu Antipas Lissu ambaye alishambuliwa kwa risasi Septemba 7, anatibiwa katika Hospitali ya Nairobi na siyo Aga Khan kama ilivyokuwa imeeelezwa hapo awali.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Chama hicho Tumaini Makene ameeleza kuwa awali walipanga kumpeleka Lissu katika Hospitali ya Agha Khan iliyopo jijini Nairobi, lakini walibadilisha mipango baadae.
“Nimesoma katika ‘media’ kwamba Lissu amelazwa katika hospitali ya Aga Khan. Hii siyo kweli. Yupo katika Hospitali ya Nairobi,” alisema.
Kabla ya kupelekwa hospitali jijini Nairobi Tundu lissu alipewa huduma ya awali katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post