UAMUZI ULIOTOLEWA NA MAHAKAMA LEO KUHUSU KESI YA MANJI

Mahakàma ya Hakimu Mkazi Kisutu ya jijini Dar es Salaam imeruhusu mfanyabiasjara Yusuf Manji na wenzake wahojiwe na Jeshi la Polisi ili kuweza kukamilisha upelelezi wa kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili.
Uamuzi huo umetolewa leo Spetemba 4, 2017 na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi ambapo alisema amefikia hatua hiyo baada ya kuandikiwa barua na Mkuu wa Upelelezi (ZCO) akiomba watuhumiwa hao wahojiwe.
Manji ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mbagala kwa tiketi ya CCM amekua akija mahakamani na kurejeshwa rumande mara kwa mara kutokana na upelelezi wa kesi hiyo kutokukamilika.
Shahidi alisema kwamba mahakama hiyo ina kila sababu ya kuruhusu watuhumiwa hao kuhojiwa kwani kila mara kesi hiyo huahirishwa kutokana na upelelezi kutokamilika, hivyo akiwazuia wasihojiwe ni kwamba upelelezi hautokamilika.
Baada ya kuruhusu watuhumiwa hao kuondoka na Koplo Dotto, hakimu huyo amesema hadi kesho (Septemba 5) ndani ya muda wa kazi, watuhumiwa wote wawe wamerudishwa mahakamani.
Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Meneja Rasilimali watu wa Kampuni ya Quality Group Ltd, Deogratius Kisinda (28), Mtunza stoo, Abdallah Sangey (46) na Thobias Fwere (43) mkazi wa Chanika ambao walisomewa mashitaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.
Katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi, Manji na wenzake wanakabiliwa na mashtaka mbalimbali yakiwamo kukutwa na mabalo ya vitambaa vinavyotumika kutengenezea sare za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Mashtaka mengine ni, kukutwa na mhuri wa JWTZ ambao uliandikwa “Mkuu wa Kikosi 121 Kikosi cha JWTZ” bila kuwa na uhalali kitendo kinachohatarisha usalama wa nchi pamoja na kukutwa na mhuri uliokuwa umeandikwa “Kamanda Kikosi 834 KJ Makutupora Dodoma” bila kuwa na uhalali kitendo kinachohatarisha usalama.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post