UKIWA NA MAMBO HAYA, UNAHITAJI MSAADA KATIKA USIMAMIZI WA FEDHA ZAKO

SHARE:

Katika maisha ya kila siku watu hufanya kila namna ili kujipatia fedha za kuwawezesha kuishi maisha wayatakayo. Watu wengi hasa wafanyaka...

Katika maisha ya kila siku watu hufanya kila namna ili kujipatia fedha za kuwawezesha kuishi maisha wayatakayo. Watu wengi hasa wafanyakazi walioajiriwa na kutegemea malipo ya mshahara mwisho wa mwezi, hujiwekea mipango ya namna ya kuitumia fesha yao kwa umakini.
Wengi hupanga bajeti na kuhakikisha kuwa wanabaki na akiba kiasi ambayo itawawezesha kufanya vitu vya dharura ambavyo huwezi kuvipanga. Mfano ugonjwa, msiba na matukio mengine kama hayo.
Ni vizuri kujiwekea akiba ya fedha katika maisha yako kwani akiba hiyo inaweza kukusaidia wakati unapokumbana na hali ngumu.
Unadhani utaishi vipi pale umeenda kazini na kukuta barua ya kusimamishwa kazi? Kama hukuwa umejiwekea akiba utakumbana na hali ngumu ya maisha mpaka pale utakapopata kazi nyinine. Je! Itakuwaje kama usipopata kazi nyingine?
Umeuona sasa umihimu wa kujiwekea akiba katika maisha? Huo ni mfano mdogo tu. Zipo hali nyingine kubwa zinazoweza kukupata na kama hukuwa umejiwekea akiba ukaishia kupata matatizo makubwa.
Wapo watu wengi wanaopata fedha nyingi katika Maisha yao lakini hawawi na mafanikio makubwa kwa sababu ya tabia zao za kutumia hovyo kipato chao.
Baadhi wanapopokea mshahara wanawaalika rafiki zao kwenda baa kunywa pombe na kustarehe. Ama mtu ananunua vitu vya gharama na visivyo vya msingi kwa kutumia fedha nyingi. Mfano kununua nguo nyingi za gharama kubwa, kwenda maeneo ya starehe na tabia zingine zinazofanana na hizo.
Hapa chini tumeonyesha baadhi ya mambo ambayo kama umekuwa ukiyafanya ama yanakukumba, basi unahitaji msaada mkubwa wa usimamizi katika matumizi ya fedha zako.
Kuchelewesha malipo
Imefika mwisho wa mwezi, lakini bado hata hujajua utakapopata kodi ya nyumba, ankara ya maji nayo inaletwa lakini huna fedha ya kuilipa. Hujakaa vizuri LUKU nayo inaisha unalala gizani kwa kukosa fedha ya kununua umeme. Haya ni baadhi tu ya matatizo yanayowakumba watu wanaotumia fedha pasipo utaratibu maalum.
Hali hii kama imewahi kukukumba ama ndiyo unapambana nayo basi unahitaji msaada wa uangalizi wa fedha zako.
Tabia ya kutoa fedha benki mara kwa mara.
Watu wenye matumizi mazuri ya pesa hupanga bajeti yao ya muda mrefu ili kuepusha matumizi yasiyo ya lazima. Kuna wakati dharura hutokea na inakulazimu kwenda benki kutoa fedha. Lakini kama una kawaida ya kwenda kutoa fedha zako ulizoziweka kama akiba benki mara kwa mara, basi ujue una matumizi mabaya ya fedha na unahitaji usimamizi wa hali ya juu katika kutumia pesa ulizonazo.
Kukopa mikopo kwa matumizi yasiyo ya msingi
Kukopa siyo jambo baya katika Maisha, lakini inabidi ujue unakopa kwa lengo gani. Ukikopa kwa lengo la kulipa gharama za matibabu yako ni sahihi, lakini unapokopa kiasi kikubwa cha fedha kwa lengo la kwenda mapumziko au kwenda kufanya starehe, hapo unahitaji kupata msaada wa karibu wa namna ya kuzitunza fedha zako.
Unapokuwa na madeni mengi kuliko uwezo wako.
Pale unapokuwa mtu wa matumizi yasiyo na msingi kama vile kwenda sehemu za starehe ambazo unatumia fedha nyingi bila kuingiza kipato chochote, utaishia kuwa mkopaji kwa kuwa utaishiwa na fedha kila mara. Hapo ndipo utakapojikuta katika wimbi la madeni ambayo hutoweza kuyalipa kwa wakati au ukashindwa kulipa kabisa na mwisho wa siku kuishia gerezani.
Unaweza kupambana na hali hii kwa kufanya kazi kwa bidi na kuhakikisha kuwa unapunguza kama siyo kuondoa kabisa tabia ya kutumia fedha katika mambo yasiyo ya msingi.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: UKIWA NA MAMBO HAYA, UNAHITAJI MSAADA KATIKA USIMAMIZI WA FEDHA ZAKO
UKIWA NA MAMBO HAYA, UNAHITAJI MSAADA KATIKA USIMAMIZI WA FEDHA ZAKO
https://3.bp.blogspot.com/-HQRWwKhIyjs/WasWkVpTO6I/AAAAAAAAeQA/QqLrmmOJzVYsyFV4K9qZ578kFBf9N__dgCLcBGAs/s1600/xbolso-jpg_152717-750x375.jpg.pagespeed.ic.NYf6lpAnBO.webp
https://3.bp.blogspot.com/-HQRWwKhIyjs/WasWkVpTO6I/AAAAAAAAeQA/QqLrmmOJzVYsyFV4K9qZ578kFBf9N__dgCLcBGAs/s72-c/xbolso-jpg_152717-750x375.jpg.pagespeed.ic.NYf6lpAnBO.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/09/ukiwa-na-mambo-haya-unahitaji-msaada.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/09/ukiwa-na-mambo-haya-unahitaji-msaada.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy