VIONGOZI WANNE WA CUF WAFARIKI DUNIA WAKITOKEA BUNGENI DODOMA

Habari zilizotufikia mapema leo asubuhi zimeeleza kuwa, viongozi wanne wa Chama cha Wananchi (CUF) wamefariki dunia baada ya msafara wao kupata ajali maeneo ya Ubenazomozi Mkoa wa Pwani.
Ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo wakati viongozi hao  walipokuwa wakitokea Dodoma kwenye sherehe za kuapishwa kwa Wabunge wapya 7 wa chama hicho baada ya gari lao kugongana na Lori.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Habari wa CUF, Abdallah Kambaya, viongozi waliofariki ambao walikuwa wakimuunga mkono Prof. Lipumba ni kutoka Wilaya ya Muheza, Tanga ambapo miongoni mwao ni Mgombea Udiwani wa Muheza Mjini, aliyefahmika kwa jina moja Uredi.
Majurihi katika ajali hiyo wamekimbizwa katika Hospitali ya Mkoa wa Pwani, Tumbi.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post