WAPEMBA KUWAPA TIZI LA NGUVU SIMBA KABLA YA KUIVAA AZAM FC

Kipute cha kirafiki kati ya Simba na Hard Rock ya Pemba kinatarajiwa kupigwa kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam ambapo ni maandalizi ya Simba kabla ya kuivaa Azam FC katika Ligi Kuu ya Vodacom.
Awali mchezo huo ilikuwa ufanyike jioni ya jana, lakini uongozi wa Simba ukaamua kuupeleka Jumapili ili kupisha maandalizi ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya wenyeji, Tanzania na Botswana.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba, Haji Sunday Manara aliomba radhi wapenzi na wanachama wao kwa usumbufu na aliwahihi kujitokeza kwa wingi Jumapili Uwanja wa Uhuru kuisapoti timu yao.
Baada ya mchezo huo Simba itakipiga dhidi ya Azam FC katika ligi kuu, hivyo mchezo huo wa kesho ni kama kupasha misuli kabla ya kuwavaa Wanalambalamba hao.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post